NENO LA UFUNUO LA WIKI HII KWA KANISA ULIMWENGUNI Nyoka asiwe mwerevu kukupita wewe

Kiongozi mkuu wa Huduma ya Neno la Ufunuo-Mtume Alam J.Kayengela akiwa kwenye sherehe za kiibada za kustarehe pamoja na Mungu kwa kushinda nyumbani mwa Mungu kuanzia asubuhi mpaka jioni-kama inavyo fanyika kanisani hapo kila siku ya ijumapili alifundisha Neno la ufunuo akasema JIHADHARI SANA NYOKA ASIKUZIDI WEREVU Mwanzo 3;1 nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama WOTE... kwa andiko hilo tu, yaweza kutosha kuku patia Ufunuo. Nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama WOTE si,binadamu WOTE. Kwahiyo kihalisi kabisa,nyoka hakukusudiwa kuwa na uerewa kuliko mwanadamu. Adamu na Eva pale nyumbani kwao bustanini waliishi wakiwa na uerewa kuliko wanyama WOTE na nyoka akiwemo.Kwa uerewa huo tu, waliweza kuwatawala wanyama WOTE na nyoka akiwemo-mwz 1;26.... Dhambi iliharibu hayo yote. Kwanini walitenda dhabi? jibu nirahisi tu,Nipale nyoka alipo wazidi werevu. Nirahisi tu,kama hivyo. HAMASIKA ZAIDI KUWA NA UEREVU KULIKO NYOKA Jiulize mwenyewe na ujihakikishie jibu. Una wezaje kumshinda adui y...