KUTHAMINI ULITHI
Kiongozi mkuu wa Huduma ya Neno la Ufunuo Mwalimu na Mtume Alam Japhet Kayengela ambaye ndiye mwanzirishi wa Huduma hiyo-katika ibada ya jana alisema;
-Ulithi nilango lako lakuingilia mbinguni
-Nimahali pale ambapo Mungu amekuweka ili kupitia hapo utafika mbinguni
-Nimahali paitwapo-kusudi la Mungu
Mtume Kayengela katika hali ya kiufunuo alitoa mfano wa watu 7 maalumu walio pewa heshima na Mungu katika historia ya Biblia-akasema,watu hao wanapatikana katika vitabu 4 tofauti
1.Ezekieli 14;12-16-hapo unamuona-Nuhu,Danieli na Ayubu
2.Yeremia 15;1-hapo unamuona Musa na Samweli
3.Marko 9;2-8-hapo,tuna muona Musa na Eliya-lakini tuna sisitiza Eliya-kwakuwa Musa tullisha mtaja
4.Mathayo 11;11-hapo tuna muona Yohana mbatizaji
-Apostle Kayengela alisema kuwa,watu hao 7 unao waona hapo wakipewa heshima ya tofauti kabisa na Muumbawao Mungu aliwataja kitofauti ili kuangalia kama unaweza kujizuia katika dunia ya kizazi hiki kuelekea kufanana nao.
NUHU-alijenga safina,kwauvumilivu mkubwa-yapasa ujiulize binafsi kuna kitugani unachofanya kwa ajili ya Mungu-achilia mbali sadaka zako za kawaida ambazo unatoa kwa kujisikia
DANIELI-nimtu aliye heshimu Ibada kuliko kitu kingine chochote-alikuwa tayali kupoteza ajira yake,marafiki,heshima ya cheo,na hata urafiki wake na mfalme kuliko kuacha Ibada.-unaweza mwenyewe ukajitazama kwenye kioo hiki jinsi ambavyo kwaurahisi sana unakuwa na udhuru na sababu kuzikwepa ibada-Mungu anakujua-unakuwa na udhuru kwenye suara la Ibada?
AYUBU-nimtu aliye vumilia mabaya,machungu,namasikitiko makubwa-bila kuliacha kusudi. Maranyingi huwezi kuelewa nikwajinsigani Mungu analuhusu upitie masikitiko kwa muda mlefu bila kuku saidia-ila umekuwa ukimsikitisha sana kwamoyo wako mrahisi kwa kukata tamaa na kuvunjika moyo kwa urahisi-hata hawezi kujivunia mtu kama wewe
MUSA-nimtu aliye kuwa na moyo mkubwa wa kuwa hurumia ndugu zake-kwasababu hiyo alidhamiria moyoni kumuonyesha Farao kwamba yuko upande HASA wa Mungu-Jiulize mwenyewe nikwakiasi gani unawasaidia dugu zako katika Bwana. Wewe unalala kwenye godoro zuri ila ndugu zako tena wakusudi moja na wewe,wanalala chini,wanatandika mkeka tu,au magunia-Je? wadhani Mungu hakuoni?
SAMWELI-nimtu aliye kulia mikononi mwa Eli,akiwa kama mtumwa wakawaida kabisa katika nyumba ya Eli-lakini alijua kwamba unyenyekevu wake siyo kwa Eli tu,bali kwa Mungu-yawezekana huwa unapata sana shida-kujinyenyekesha kwa mchungaji wako labda kwasababu unamzidi kipato au umri na hata elimu hii ya kawaida
ELIYA-nimtu aliye pigania sana imani ya Mungu aliyekuwa anamtumikia-alipigania kusudi,hata kama ilibidi kupambana na manabii 400 haikujalisha.Yeye hakukubali kusudi la Mungu wake kuaibishwa au kukosa kitu furani ambacho kitasababisha kusudi kuaibika. Binafsi huwa una utayali gani kulitetea kususudi la Mungu wako kwa namna yoyote? inafurahisha kwamba,Mungu anakujua vyema
YOHANA MBATIZAJI-nimtu aliye mtumikia Mungu katika mazingira magumu sana ya kukosa chakula kizuri,mavazi mazuri,starehe nzuri za mijini n.k ili kuandaa njia au mtembeo wa Bwana Yesu duniani. Sijui jinsi gani unavyo jighalimu kwa pesa zako na mali zako ili kuhakikisha babayako wa kiroho unamuandalia mazingira yakumfanya amtumikie Mungu vizuri-wengine wanasubiri waambiwe lakini Mungu anakujua
Mtume kayengela
ALISEMA-
Kwamtu ambaye hana akili ya kiroho,mambo haya anayaona yakawaida tu,
-Ndiyo maana wakati mwingine tunapo tangaza michango watu huangalia tu kutimiza malengo yao bila kushituliwa na hilo- huku wakidhani hilo nijambo la kawaida tu.
KWANINI UNATAKIWA UTHAMINI ULITHI AU KUSUDI?
1.Urithi ni asiri ya nguvu zako-Waamuzi 16;5-22
-Apostle Alam alisema-
Asiri ya nguvu za samsoni ilikuwa nywele zake-ambapo wewe asiri yanguvu zako nilile kusudi au urithi
2.Unatakiwa kuuthamini ulithi kwasababu nikupitia hapo,hatma yako inaandaliwa-Ayubu 8;7-Mtume Kayengela alisema-Maisha ya mbarikiwa aliye katika kusudi na si,dhehebu au dini-yamefananishwa na Wingu dogo linalo lingana na kiganja cha mkono wa mtu-1wafalme 18;41-44-yanaongezeke kimiujiza muda wowote na kusababisha baraka kwa watu wengi
3.Bila ulithi -huna shamba lakupanda mbegu zako za kisadaka-muhub 11;4-16-Mtumishi alisema kwamba,watu wengi wanapoteza pesa zao kwa kuziweka mahali ambapo sipo,huku shetani akiwadanganya kwenye akili zao kwamba wanapanda mbengu kwa Mungu. Mtego huu siyo wengi wameukwepa. SIYO WENGI
ONYO
USIKAE KWENYE KUSUDI KAMA MCHUNGULIAJI
1SAMWELI 6;19-21-Ona mistali hiyo-watu maelufu waliangamizwa na Mungu si,kwa kuwa wamezini au kuiba-hapana-Bali nikwasababu wali chungulia kwenye sanduku-unajua sanduku laleo nikusudi.
kuchungulia nikama kuwa shabiki tu, kwenye kusudi
-shabiki kazi yake nikukosoa tu, nakuangalia wale wano shindwa-wale wanao jidhania sana kwamba wameelimika ndo huwa wanatumiwa sana kwenye eneo hili-
Zab 96;2 usipo jihusisha na kusaidia uenezwaji wa injili kwenye kusudi lazima uelewe kwamba wewe ni shabiki tu,kwenye kusudi hata kama unasema unampenda sana Mungu
URITHI-ndio unao kufikisha uzeeni ukiwa bado una zaa faida-zab 92;12-14
Ubarikiwe
Nina kukaribisha kwenye Kusudi la Neno la Ufunuo
sura ya nje ya ukumbi wa muda ikionyesha na eneo ambalo Apostle Kayengela hulitumia kwa ajili ya kukutana nawatu wanao hitaji ushauri na maombezi binafsi
huduma ya maombezi inaendelea kushika kasi katika ibada hizo zinazo anza as.mpaka jioni
Comments
Post a Comment