Leoleoplus,com

Machapisho

1 . KUPIGA VITA VIZURI VYA IMANI DHIDI YA JESHI OVU LA HILA ZA SHETANI

Kitabu hiki chenye kurasa zaidi ya mia moja  hamsini  kina mambo makuu 8 yasiyoweza kupuuzwa na mtu yeyote anayepumua hapa duniani.

1. Kimeelezea kwa kina kuhusu majeshi maovu  ya hila  za shetani ambayo yametumwa na kusambazwa  hapa duniani  kwa kazi  maalumu  yakuliangamiza  kanisa. Kimeyafunua  wazi majeshi 31 ambayo  ibilisi ameyatuma hapa duniani  toka kuzimu.

Haya ni maelezo kwa kifupi kuhusu  baadhi  ya maagizo  maovu juu ya majeshiya ibilisi yakiamriwa na shetani mwenyewe Jeshi  ovu la mafarakano- Shetani  alitokea mbele ya jeshi hili  akaliagiza  nakuliambia huku akionesha msisitizo na umakini  akasema-Nendeni mkafarakanishe  maana mimi sitaki umoja. Mnafahamu , umoja wao ni mkuki unaonipiga ubavuni na kunifanya  kulegea.

Ninawatuma nyie mkashambulie  mahali popote penye umoja. Alipo maliza kusema hayo, akalipita jeshi hili kuelekea lingine.
Haya mapepo yanapoondoka  kutenda kazi yanaenda taratibu yakiwa  yametoa  macho kwa umakini wa hali ya juu sana, kuangalia wapi kuna umoja.

Jeshi la uadui- Shetani  alitokea mbele ya jeshi  hili  akaliagiza akasema:- Nendenimkasababishe kazi yenu kuonekana kila  mahali (uadui) mtakaposababisha hiyo kazi kuonekana ndipo  tutafanikiwa kusababisha mgawanyiko; kitu ambacho  kitasaidia sisi kuwafanya wasiwe na ile hali ya kushirikiana ilituweze kusababisha  uharibifu  wetu kwa raha sana  bila kubugudhiwa wala kuzuiliwa  na yeyote. Baada ya  hayo maagizo, shetani alisonga mbele zaidi  kwenye majeshi mengine.

Jeshi lakuandaa watoto wakristo kuwa watumishi wa shetani-Alipofika shetani kwenye jeshi hili aliyageuza macho yake  huku na huku akiliangalia jeshi hili kwa mkazo, kana kwamba anahisi kuna mapepo yamepungua kwenye hili jeshi ndipo akaliambia;- myaenda kufanya kazi yangua hii,  bila haraka lakini kwakumaanisha .

Nawapa  vifaa na nyenzo, zitakazo wawezesha kuhakikisha mtoto asilelewe na kukuzwa  katika maadili sahihi ya Mungu wao.Japokuwa kazi yenu ni ya muda  mrefu lakini inafaida kwangu kwa kuwa  napata jeshi  litakalonitumikia  kwa nguvu. " Akiisha  kusema hayo  akaondoka. Jeshi hili lilielekezwa  kwa watoto wenye umri wa kuanzia miaka 12 hadi 23.

NB: Jitahidi upate kitabu hiki, utapata mambo mengu ndani yake.


2 . MAOMBI YAKUSAMBARATISHA MAJESHI YA ROHO ZA KICHAWI.

Kitabu hiki kina kurasa zaidi ya mia moja na thelathini.

 Kitabu hiki kina mambo mengi mazuri yaliyo ya muhimu sana kwa kila  mtu anayetaka kuishi duniani akiwa mshindi dhidi ya  ya majeshi haya sumbufu ya  roho za kichaw Kimeelezea wazi  baadhi ya  makundi  matatu ya watu wanaoishi hapa duniani, kwamba kundi la kwanza ni watu ambao wanaishi kwa kubahatisha yaani wanaishi katika namna ambayo, wachawi wanapoamua  kuwafanyia kitu chochote wanawezakufanya katika kundi hili wapo maskini, matajiri, wasomi n.k.

 Ni katika hili kundi  ndipo wachawi huchagua  watu wakuwatoa makafara na kuwafanya  kuwa watumwa wakichawi bila wahusika kujijua hata kidogo. Kundi la pili ni lile  la watu wanaoishi duniani  kwa kujitahidi. wanaishi kwa kusumbuliwa  na wachawi japo hawashindwi moja kwa moja. Hawa ni watu  ambao wanaelewa fika kwamba wachawi wamewazuilia baraka zao , lakini hawajui lakufanya. Mara nyingi hushambuliwa  na wachawi usiku wakiwa  usingizini au wakiwa macho.

Kundi la tatu ni lile ambalo linaogopwa sana  na wachawi. Hili  kundi  ni kundi  sumbufu sana kwakuwa hata wachawi wenyeqe na bosi wao  shetani  wanalifahamu kundi hili. Shetani analiogopa kundi hili japo haachi kulijaribu kwa maana yeye ni  mjaribu. Ni kundi ambalo linaonekana  kama mianga ya moto duniani.

Kitabu hiki kimeelezea  kwa kina jinsi  ambavyo unaweza ukawa mmoja wa watu  wa kundi hili sumbufu kwa wachawi .Mapambazuko ya alifajiri  moja ya tarehe 14.11.2011 saa 12:55 usiku siku ya Jumapili ndipo mtumishi huyu Mwalimu na Mtume Alam Kayengela  alipoletewa ujumbe huu mahususi.

Yapo mambo mengi sana  utakayojifunza ndani ya kitabu hiki.


3 . CHUKUA NAFASI  YA KUJITAMBUA WEWE NI NANI NDANI YA KRISTO.

Kitabu hiki chanya kurasa zaidi ya mia moja na kumi.  kimesheheni hazina nyingi sana  za  masomo yasiyopungua thelathini yanayomfanya mtu kwa namna yoyote ajitambue  kwa undania  sana  yeye  ni nani ndani ya Kristo Yesu. Katika kitabu cha Yohana 1: 19-34 mafarisayo walituma watu kumuuliza Yohana ilikujua yeye  ni nani. Utambulisho wake ulidhihirisha  wazi jinsi yeye binafsi  alivyokuwa anajitambua kwamba yeye  ni nani ndani ya Kristo yesu.
 Walimuuliza - Wewe ni Eliya? Akasema  hapana. Wewe ni Yesu? Akasema hapana.- na kadhalika. Baadae aliwajibu nakuwaambia" mimi nisauti ya mtu aliye nyikani, inyoosheni njia ni njia ya bwana..." Je! Kwanini hakusema mimi ni Yohana mwana wa Zakaria? Hapa alikuwa anatuonesha  wazi jinsi yeye mwenyewe alivyojitambua ni nani ndani ya Kristo.

Baada yakukisoma kitabu hiki utajigundua  kwamba  wewe ni zaidi ya vile ulivyojifahamu. Utapata  mwinuko  mpya  waliroho kwakusoma kitabu hiki  cha kuchukua  nafasi yakujitambua  wewe ni nani ndani ya kristo. Utafahamu mengi kujihusu wewe kupitia masomo haya 30 yakujitambua wewe ni nani ndani ya Kristo Yesu, yaliyofunuliwa kwenye kitabu hiki cha muhimu na cha lazima kwa kila mtu.

4 . HAYA NI MAOMBI YALIYOTHIBITISHWA

   (MWILI WAKO NI MNYORORO MKUU UNAOKUFUNGA USIWEZEKUTEMBEA NA MUNGU KATIKA  WINGU LA UPAKO WA MAOMBI MWAKA HUU)

Kitabu cha haya ni maombi yaliyothibitishwa  kinakuwa sasa ni  kitabu cha aina tofauti na vile  mtu anavyoweza kukidhania ikiwa baada yakukisoma. Pindi utakapoanza kusogeza kurasa moja baada ya nyingine kwa kusoma kitabu hiki, haraka utagundua kwamba, ni kitabu kinachohusu maombi lakini kikiwa si cha kawaida. Ndiyo! Hilo unaweza kulitarajia.Kitabu hiki kimetoa maelekezo sahihi na kwa  uwazi , jinsi unavyoweza kutembea na Mungu katika wingu la upako wa maombi mwaka huu.

Kimefafanua  mambo mengi yakuhusu maombi mfano ni maombi ya aina ganai unayotakiwa kuwa nayo unapoanza mwaka , mwezi ,wiki, siku hadi saa.Kimetoa muongozo pia katika mambo yafuatayo;
 Mwaka wenye miezi kumi na mbili unatakiwa uombe siku ngapi?
  •   Mwezi wenye siku 30 au 31 unatakiwa uombe siku ngapi?
  •  Wiki yenye siku saba unatakiwa uombe siku ngapi?
  •  Siku yenye saa 24 unatakiwa uombe muda gani?
  •  Masaa yenye dakika 60 unatakiwa utumie muda gani katika kuomba.

Ndani ya kitabu hiki pia yameainishwa mambo yanayoweza kuwa kikwazo na kizuizi cha majibu ya maombi yako.
Kila mtu anahitaji hiki kitabu.


5 . KUITAMBUA SAUTI TYA MUNGU.

(sauti ya Roho mtakatifu ya maonyo kwa wachungaji na awatumishi wote wa kizazi hiki ulimwenguni).
 Tarehe 18.09.2011 siku ya Jumamosi  saa 2:00 asubuhi ndipo Mungu alipomletea ujumbe huu mtumishi wa Mungu na kupewa agizo la kuandika  na kuweka  kwenye jarida chache za kitabu hiki.

 Ujumbe huu  alipoupata  mtumishi  wa Mungu ulimfanya  Kuugua Rohoni  karibu wiki mbili , hasa anapokumbuka  msisitizo  wa maonyo ya roho Mtakatifu kwa wachungaji  na watumishi wote wa kizazi  hiki ulimwenguni. mara nyingi aliandika  kitabu hiki  akiwa analia machozi. Kitabu hiki kina maonyo tisa tu  ambayo  mtumishi wa Mungu aliyaandika moja baada ya  jingine kwakusikiliza kwa makini asije akaandika tofauti na yale ambayo Roho wa Mungu angetaka yawafikie kwa ukamilifu watumishi wa Mungu

wote wa kizazi hiki ulimwenguni. KILA MCHUNGAJI AKIPATE KITABU HIKI.
Kila aliyekipata kitabu hiki anaweza akakiri  wazi kwamba ,siyo mawazo ya mwandishi aliyepangilia  kwa utaalamu  usio wakawaida  maneno ya kitabu hiki.
  •  Unapoanza kusoma kitabuhiki  mwanzo  mpaka  mwisho, unakuwa  umeshaielewa sauti  ya Mungu inayokuwa  inazungumza na wewe kupitia kitabu hiki.
  • Hii ni dalili ya Mungu kuwapenda watumishi wake  wakizazi  hiki  ulimwenguni, kwamba  anaweza akawaonya .- Huu  ni upendo .

NB: Kila mtumishi akipate kitabu hiki.


6 . ZITAMBUE BAADHI YA ROHO 76 ZINAZOTESA KIZAZI HIKI.

  Kitabu hiki  ni kitabu maalumu kilichobainisha  baadhi ya roho 76 zinazotesa  kizazi hiki.

  Baadhi ya hizo roho 76 zinazotesa kizazi hiki , ziliwahi kutesa pia vizazi vingi vya mwanadamu tangu alipowekwa duniani katika karne zilizopita.

 Roho zote 76 zilizofunuliwa katika kitabu hiki, zimewekwa wazi  kwa Neno kila roho ikifunuliwa na andiko  jinsi ilivyotenda kazi  kwa kumtumia mtu wa vizazi  vile  na jinsi unavyoweza ukaibainisha kwa uwazi inapotenda  kazi katika  kizazi chetu hiki. Mfano;- Roho ya shimei:

 katika kitabu hiki hii ni roho ya 69 kati ya roho 76 zilizobainishwa  katika kitabu hiki.

Unaposoma katika 25 Samweli 16: 5-14 unaona wazi  mtu aliyeitwa  kwa jina la

shimei jinsi alivyohusika kutukana watumishi wa Mungu, na kwakuwarushia mawe, na kujaribu  kufanya ubaya  wa kila namna. Roho hiyo ya shimei haikuishia hapo , katika kipindi cha Daudi  bali inatenda kazi hata sasa  kwa kuwatumia kina shimei  wanyakati hizi za kizazi hiki. Roho hii bado inamtumia shimei kutukana na kulaani watumishi wa Mungu wakweli wakizazi hiki. Inarusha mawe ya maneno mabaya  kila siku kwa watumishi wakweli wa Mungu wakizazi hiki.
Ni katika umuhimu usioweza kupuuza  kwamba kitabu hiki unatakiwa  kuwa nacho.


7 . BAADHI YA NJIA 30 AMBAZO MUNGU ANAZITUMIA KUSEMA NA WATU.
  •    Usiku wa tarehe 16..07.2010 saa 2:05 mwandishi akiwa  safarini  ndani ya basi alipewa ujumbe  wa kitabu  hiki.
  • Ni kitabu kizuri sana kilicho na siri za Mungu za kumfanya mtu kwa urahisi aweze kutambua sauti ya Mungu kwa namna fulani.
  •   Mara utakapokuwa umesoma kitabu hiki na kukimaliza kwa usahihi  utaanza mwenyewe kupata uhakika wa dhati kwamba unaweza kusikia Munu  akiongea na wewe aidha kwa njia ambayo hapo kabla hukuijua.
  •   Muhtasari mfupi wa kitabu hiki - hebu ukupe hali yakujua kwamba kwa namna yoyote ile kitabu hiki, kimeshehenii hazina nzuri zilizo za Mungu kwako binafsi.
  •   Asilimia kubwa sana ya idadi ya wakristo humu ulimwenguni waliowahi kuishi na wale waliopo mwelekeo wa ufahamu wao kuhusu njia ambazo Mungu huzitumia kusema na watu ni kama zifuatazo;
  •    Sauti ya wazi
  •    Kwa njia ya ndoto
  •    Kwa njia ya maono
  •    Kwa njia ya dhamiri au amani ya Kristo
  •   Kwa njia ya manabii au malaika

- Hizo ni baadhi ya njia ambazo watu wanhisi kuwa Mungu anawezakuzitumia kusema nao.
  •    Njia zingine 25 bado zimesitirika lakini kitabu hiki kimeweka wazi njia hizo kwa usahihi zaidi.


8 . CHUKUA TAHADHARI JUU YA MNYAMA KATILI ACHINJAE NA KUANGAMIZA (KIBURI).
  •    .Kitabu hiki kimetoa tahadhari kubwa juu ya kile kilichotafsiriwa kama mnyama katili- ambaye mnyama huyo katili ndiye kibri mwenyewe.
  •    Kiburi ni roho ya mnyama wa ajabu sana. Ni mnyama katili. Ni aheri utekwe na kingine chochote maana unaweza siku moja unaweza ukafunguliwa, kuliko kutekwa na mnyama huyu kiburi ambaye anakufanya Mungu kuwa kinyume chako.
  •    Mnyama huyu kiburi anakufanya Mungu akupinge kwa kila namna- 1 Petro 5:5.
  •   Ujumbe mzito ulioko ndani ya kitabu hiki,mtumishi mwalimu na mtume, Alam J. Kayengela ambaye ndiye mwandishi wa kitabu hiki, kwa neema ya Mungu alifunuliwa na Mungu tarehe 11-09-2007 akiwa Kibaha Mkoa wa Pwani kupta ujumbe huu, ujumbe wa kitabu hiki umechapwa sehemu ya kwanza hadi ya tatu.
  •    Kiburi ni mnyama katili mwenye mikono tisa. Ana macho makali yakuona mbali. Anaukubwa ya mfano wa Tembo. Wepesi wake wakukamata mawindo ni kama chui.
  •    Kitabu hiki kimeainisha wazi maeneo makuu matano ambayo mnyama huyu kiburi anapenda kutembelea ili kumkamata mtu ( mawindo).
  •    Pia kitau hiki kimefafanua kwa uwazi mikono tisa ambayo mnyama huyu kiburi anayotumia kuwakamatia watu (mawindo) ilikuwapokonya.
  •   Mungu anpokuinua juu sana hata umbali wa maili milioni kisha kwa upande wako ukajiinua mwenywe hata umbali wa futi moja tu, hiyo futi moja itaathiri umbali wote wakilele ulichokuwa umekwenda kisha maili zili zitakuwa za kwenda chini na kushushwa- haya yakiwa ni matokeo yakukamatwa na mikono yote tisa ya mnyama Kiburi.
  •   Kitabu hiki kwa undani zaidi kimefundisha unyenyekevu wa kweli NB:

Tahadhari usikose nakala ya kitabu hiki.

Comments

Popular posts from this blog

NENO LAUFUNUO LA LEO tazama Ayubu 8:7"Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa mdogo,lakini mwisho wako ungeongezeka sana"NENO LA UFUNUO LASIKU YAKO LEO. MUNGU ANAKUTAKA USIWE NAMAWAZO YA KUDHARAU MWANZO WAKOMDOGO. KWAMAANA TABIA YA MUNGU NIKWAMBA,YEYE HUWA HAUDHARAUMWANZO MDOGO. HATAKAMA NIMWANZO MDOGO YEYE HATAUDHARAU. "Mungu alianza na mwanadamu mmoja,leo hii wako mabilioni. Yesu alianza na wanafunzi kumi nawawili,leohii anawafuasi wengi hata hawana idadi maanawengine walishatangulia mbinguni. Historia yamakanisa mengi Africa na ulimwengu kwaujumla,yalianza namwazo mdogo sana lakini yamekuwa makubwa nayakushangaza."KILA MWANADAMU CHINI YAJUA ANAPITIA UZOEFU HUU WA KIPINDI CHAMWANZOMDOGO.LEO INABIDI UJIULIZE UKO KWENYEMWANZOMDOGO WAJAMBO GANI? JE UKO KWENYE MWANZOMDOGO WA KUANZISHA KAZI YAMUNGU? JE UKO KWENYEMWANZOMDOGO WANDOA? UKO KWENYEMWANZO WABIASHARA? UKO KWENYE MWANZO WA OFISI MPYA? UKO KWENYE MWANZO WAUCHUMBA? UKO KWENYE MWANZO WA AJIRA? UKO KWENYE MWANZO GANI? TAZAMA zekaria 4:10"maana ninani aliyeidharau siku yamambo madogo?.....OK. UNAONYWA! USIDHARAU MWANZO MDOGO ULIO NAO LEO. USIVUNJWE MOYO NAMWANZO MDOGO. USIKATISHWETAMAA NAMWANZO MDOGO.USIJIWAZIE VIBAYA KWASABABU YA MWANZO WAKO MDOGO. LEO,PIGA MOYO WAKO KONDE UCHANGAMKE MWISHO WAKO NIMZURI. MWISHO WAKO NIMKUBWA. POKEA NENO HILI LAUFUNUO ALILO KUTUMIA MUNGU SIKU YALEO.JITAHIDI UJE KANISANI UPATE MAELEKEZO ZAIDI. HUDUMA YA NENO LAUFUNUO CHINI YA MWANGALIZI MKUU MWL NA MTUME ARAM J.KAYENGELA IMEFANYIKA BARAKA SANA YAKIROHO NAKIMWILI KWAWOTE WALIO FANIKIWA KUJIUNGA RASMI. NIHUDUMA YAKIROHO YENYE UHUISHO MPYA KATIKA SIKU HIZI ZA HATALI AMBAZO KANISA LIMESAHAU UPENDO WAKWANZA.KANISA LIMEPOA.WATU WAKO MOTO KISIASA ILA KIROHO WAMEPOA KABISA.NINYAKATI ZA YEYE ALIYE NASIKIO AYASIKIE HAYA AMBAYO ROHO ANAYAMBIA MAKANISA.HERI MWENYE SIKIO LAKUSIKIA SASA. NIMUDA WAKO WAKUJA KWENYE NENO LAUFUNUO IKIWA ULIMUULIZA MUNGU AKUONYESHE NIWAPI UENDE. SIMAMA KWAMIGUU YAKO NAUCHUKUE HATUA. 0763359745/0712583194

MFULULIZO WA MAFUNDISHO YA APOSTLE ALAM J. KAYENGELA KWENYE KONGAMANO LA SIKU NANE ARUSHA TANZANIA (TAREHE 5-12 MWAKA 2013)

SEHEMU YA PILI