NGUVU 4 ZINAZO MUHAMASISHA MWENYE HEKIMA KUENDELEA KUJITOA KIKAMILIFU KWENYE KUSUDI AU KWENYE MAPENZI YA MUNGU-sehemu ya 4 UNYAKUO
Apostle Alam-Akihubiri jana kanisani hapo-alianza kwa utangulizi
AKASEMA
Kuna nguvu 3 zinazo wasukuma walio poteza mapenzi ya Mungu katika maisha yao
-Kumbuka kwamba siyo wote walio fanikiwa kuya ishi mapenzi YaMungu-kwasababu hiyo ndo maana kuzimu yamoto inapokea watu kila siku. Malanyingi wanao shangaa pale wanapo jikuta wako kuzimu ya moto niwale walio jidhania kuokoka. Waliishi kawaida tu,na waliishi kiholela huku wakipafanya mbinguni kuwa mahali parahisi kupafikia.Walikuwa nawokovu feki huku wakiogopa kuchukua hatua za kimaamuzi kujighalimu maisha ya wokovu wa kweli.
Apostle Kayengela ALISEMA
NGUVU HIZO 3 NIZIPI?
a.Unafuu wa maisha au utajiri-Hufanyika kuwa nguvu inayo muhamasisha mtu huyu aliye poteza mapenzi ya Mungu maishani mwake kuhamasika kujitoa kwa Mungu au kwenye mambo ya Mungu-Kiongozi huyo mwanzirishi wa Huduma ya Neno la Ufunuo-ALIONGEA KWA MSISITIZO NAKUSEMA-
-Binafsi unatakiwa kujiuliza-NI NINI HASA KINACHO KUSUKUMA KUFANYA HAYO UNAYO YAFANYA KWA MUNGU?
-Kukosa jibu la swali hilo-nisawa na kuishi na bomu chumbani mwako ambalo hivi karibuni lina kwenda kulipuka
b.Umaalufu,vyeo,madaraka,na sifa-hii ninguvu yapili yauhalibifu inayo wasukuma watu wengi walio poteza mapenzi ya Mungu kwenye maisha yao kujitoa kwa Mungu-hapa ndipo unapo kuta sababu kwanini watumishi wengi waMungu niwa ganga wakienyeji wanao tenda kazi kwa kifuniko cha Jina la Yesu Krito-Bila Neno la Ufunuo siyo rahisi kuwa tambua wahuni hawa wakiroho,wataalam wakuigiza
c.Unafiki,na Ushawishi-hii nayo ninguvu ya uovu inayo wasukuma watu waliopoteza mapenzi ya Mungu maishani mwao
-Anajitoa ili amshawishi mtu furani au aonekane mtu muhimu kwamtu furani-kama mchungaji wake,au muajiri wake n.k-Nataka uelewe kwamba,uta kuwa umeptoka ikiwa nia yako nihiyo katika kujitoa kwako kwa Mungu. Umepotoka.
MTUME KAYENGELA-alibainisha kuwa,nguvu inayo wasukuma wenye hekima kujitoa kwenye kusudi au kwenye mapenzi ya Mungu ni;
4.UNYAKUO
-Unyakuo ni nini?
a.Unyakuo nitukio la kuhamishwa toka duniani kwenda mbinguni litakalo fanyika kwa kushtukiza-1Thes 4;13-18
b.Nitukio litakalo tokea ghafra bila taalifa-kwa mfano wa umeme-math 24;27-36 na mst 39
c.Nitukio la kimuujiza litakalo fanyika hivi karibuni,likiwa mfano wa kupaa kwa Bwana Yesu-matendo 1;6-12
-katika kipengele hiki Mtumishi alieleza kwa ufupi kuhusu miujiza 5 yenye kufunua nguvu uwepo na ukuu wa Mungu
AKASEMA
1,UUMBAJI
2.KUZALIWA KWA YESU KRISTO
3.KUFUFUKA KWA YESU
4.UTAWALA WA MIAKA 1000 UTAKAO ANZA HIVI KARIBUNI
5.UNYAKUO WA KANISA
-Haya nimambo makubwa ambayo BILA Imani haiwezekani kuyaamini au kuya kubali.
KWENYE UNYAKUO KUNA NINI?
1.Kuna kunyakuliwa au kuachwa-maana yake lazima uamini kwamba,SIYO WOTE WATANYAKULWA
2.Utusi-tusi-Sefania 1;14-18-nini hasa maana ya Utusi tusi?
Apostle Kayengela alitoa fafanuzi kwa ufupi juu ya maana halisi ya utusi tusi wa siku ile ya unyakuo
AKASEMA
UTUSI TUSI WA SIKU ILE YA UNYAKUO NIKWAMBA;
-Kwanza kabisa,sikuile ya unyakuo nisiku kubwa kipekee. Siku hiyo kuta kuwa na mparanganyiko mkubwa sana ambao haukutarajiwa.
AKASEMA
-Fikilijuu ya rubani wa ndenge aliye okoka sikuhiyo anapo nyakuliwa ndege ikiwa juu kabisa kwenye anga la kimataifa-nini kita tokea kwandege hiyo na abiria wake
-Unajua siku ile wafanya biashara wadogo wadogo-watagombania nguo za wapendwa walio nyakuliwa
-Fikiri juu ya dereva wa tren aliye okoka siku hiyo ananyakuliwa akiwa kwenye mwendo kasi ajabu nini kitaendelea
-Bila kumsahau nahodha wa meli aliye jaza abilia nini kitatokea atakapo nyakuliwa?
-Ndiyo maana Mungu anasema siku ile ya unyakuo niya utusi tusi
Mwenye hekima,anajitoa kwa Mungu kwa kushinikizwa na ufahamu wake sahihi juu ya UNYAKUO
Comments
Post a Comment