NENO LA UFUNUO LA WIKI HII KWA KANISA ULIMWENGUNI Nyoka asiwe mwerevu kukupita wewe
Kiongozi mkuu wa Huduma ya Neno la Ufunuo-Mtume Alam J.Kayengela akiwa kwenye sherehe za kiibada za kustarehe pamoja na Mungu kwa kushinda nyumbani mwa Mungu kuanzia asubuhi mpaka jioni-kama inavyo fanyika kanisani hapo kila siku ya ijumapili alifundisha Neno la ufunuo akasema
JIHADHARI SANA NYOKA ASIKUZIDI WEREVU
Mwanzo 3;1 nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama WOTE...
kwa andiko hilo tu, yaweza kutosha kuku patia Ufunuo. Nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama WOTE si,binadamu WOTE. Kwahiyo kihalisi kabisa,nyoka hakukusudiwa kuwa na uerewa kuliko mwanadamu. Adamu na Eva pale nyumbani kwao bustanini waliishi wakiwa na uerewa kuliko wanyama WOTE na nyoka akiwemo.Kwa uerewa huo tu, waliweza kuwatawala wanyama WOTE na nyoka akiwemo-mwz 1;26....
Dhambi iliharibu hayo yote. Kwanini walitenda dhabi? jibu nirahisi tu,Nipale nyoka alipo wazidi werevu. Nirahisi tu,kama hivyo.
HAMASIKA ZAIDI KUWA NA UEREVU KULIKO NYOKA
Jiulize mwenyewe na ujihakikishie jibu. Una wezaje kumshinda adui yako anaye pambana nawe kila siku nawakati anakuzidi uerewa? Ok, unalo jibu. Utarajie nini ikiwa nyoka au shetani anakuzidi ufahamu? KUSHINDWA
NALIONYA KANISA DUNIANI KOTE-CHANZO CHA KILA TATIZO SIYO MAPEPO TU,ILA NIKUZIDIWA UEREWA NA NYOKA
Utakuwa umewahi kusoma vizuri kitabu cha Kutoka 1;10? inasema-Haya, natuwatendee kwa akili....
Elewa kwamba,adui hatendi kijinga-ana kutendea kwa akili. Sasa ni OLE KWAKO-usipo elewa niakili gani anayo itumia ili kuku tendea.Wengi hawaelewi kabla adui hajatenda,nahuko ndiko kukosa maalifa.Unapo gundua baada ya adui kutenda hiyo niarama yako thabiti kwamba adui anakuzidi uerewa.
Utawezaje kudhani kwamba,itakuwarahisi kwako kumshinda shetani nahali anakuzidi uerewa?.
Nataka kanisa ulimwenguni kote lijue kwamba,CHANZO CHAKILA TATIZO NIILEHALI YAKUZIDIWA UEREWA NA NYOKA.NI ILE HALI YA KUZIDIWA MAALIFA NA ADUI.
Nyoka anapo kuzidi uerewa,atafanya chochote atakakachopenda kufanya kwako usijidhanie kwamba maombi tu,yatamzuia-hapana. Kanisa haliangamizwi kwa kukosa maombi. Lina angamizwa kwa kukosa maalifa-yaani UEREWA.
Tafadhari amini jambo hili-BILA NENO LA UFUNUO HUWEZI KUPATA UEREWA WAJUU WAKIROHO.Usisahau pia kwamba,SI,kila mchungaji amepewa Neno la ufunuo.
kuhusu usomaji wa vitabu
Apostle amekuwa akisisitiza nakulishauri kanisa ulimwenguni kujitahidi kusoma vitabu vya kiroho ambavyo vimeandikwa na watumishi ambao kwa uhakika maisha yao yana muunganiko usio na mashaka na Roho Mtakatifu. Alisema kwamba;

amekuwa akipokea shuhuda za kweli zinazo tokana nawale wanao amua kununua pia vitbu vyake-alisema kuwa,hapigi debe ili vitabu vyake vinunuliwe lakini anampa nafasi mtu mmoja mwenye uerewa kuona umuhimu wa kujipatia vitabu hivyo. Ameandika zaidi ya vitabu 13 baadhi ya mihtasali yavitabu hihivyo,uki tafuta kwenye neno machapisho utaiona.
Namna ya kupokea neema toka kwenye usomaji wa vitabu hivyo
-Alisema;

Unapo soma kwakutarajia kumsikia Mungu akiongea kupitia kitabu hicho-Utamsikia. Unapo soma ukiwa katika hali yakawaida,itakuwa hivyo hivyo kawaida
JIFUNZE KUSOMA ALAMA NANYAKATI AMBAZO NYOKA ANAPOKUWA MWEREVU KULIKO WEWE
1.Pale anapo kubebesha mzigo wa kukosa furaha na amani-kut 1;11
-kukosa furaha na amani lisizaniwe kuwa jambo lakawaida. Pia haliwezekani kulifaidi bila Neno la Ufunuo
2.Wakati unapo ona uhalali kulipiza kisasi
3.Unapo anza kutwikwa mzigo wa uzinzi nakuanza kukosa hofu juu ya hilo
4.Unapo anza kuona maisha ya ibada kwako nikero na mahangaiko
5.Unapo bebeshwa mzigo wamgandamizo wa kukata tamaa kwenye maisha hasa kwenye kusudi
6.Unapo jisikia salama kutokufika ibadani
7.Ukianza kususia baadhi ya vipindi vya ibada-na kuacha kutafuta amani kwenye Neno, Amani iko kwenye Neno. Wengine kwa kutokujua,wakati wanapo jisikia hawana amani hukimbilia kwenye maombi,wanashangaa hata baada ya maombi hawana amani. Amani iko tu,kwenye Neno HASA lile la Ufunuo
kwamawasiriano zaidi
alamkayengela@yahoo.com
mlkayengela@gmail.cm
simu; 0763359745 au 0712583194
Comments
Post a Comment