Mtumishi
Mwalimu na Mtume Alam J. Kayengela ni Mkurugenzi mkuu mwanzilishi wa huduma hii.
Baada ya Mungu Kumpa maelekezo alimtuma toka Mkoani Kigoma kuja kuanzisha huduma hii mnamo mwezi wa tatu mwaka 2010 Dar Es salaam katika manispaa ya Temeke eneo la Yombo Vituka.
Neno La Ufunuo:
Neno hili linatoka katika kitabu cha 1 Samweli 3:1 (b) "Na neno la Bwana lilikuwa adimu siku zile ; hapakuwa na mafunuo dhahiri". Kama hivi tungesema mahubiri na mafundisho yalikuwepo lakini yakiwa hayana ufunuo.
Makuhani walitoa hotuba zao kwa usahihi na mpangilio wa dhati, wakinukuu torati ya Musa kwa ulinganifu na sahihi lakini hapakuwapo na mafunuo dhahiri.
Kwahiyo Neno pasipo ufunuo dhahiri ni andiko lisilo na pumzi ya Mungu 2 Timotheo 3:16 " Kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho na kwa
kuonya watu makosa yao, na kwa kuongoza...". Hii inamaana ya wazi kwamba kila andiko lisilo na pumzi ya Mungu halifai kwa matumizi yoyote ya kiroho. Hiyo ni kwa sababu andiko huua bali roho analihuisha.
1Korintho 14:30" lakini mwingine aliyeketi akifunuliwa neno....siku zote, Neno la ufunuo mtu hupewa (hufunuliwa) na Mungu mwenyewe. Ndivyo Yesu alivyomwambia mtume Petro". Heri wewe Simoni Bar-Yona, kwakuwa mwili na damu havikukufunulia hili ; bali Baba yangu aliye mbinguni, Mathayo 16:17". Yesu Kristo kwa kumwambia hivyo Petro alimaanisha pia kwamba, "Mwili na damu au mawazo ya kibinadamu yanaweza kufunua mahubiri japo yanakuwa hayana nguvu ya kumpa mtu uhai". Ila kumdumaza mtu kiroho na kimwili.
Huduma ya Neno la ufunuo ya Uongozi wa Roho Mtakatifu kupitia Mwalimu na Mtume Alam J. Kayengela ianshughulika na haya yafuatayo:-
1. Kumfanya mtu alijue neno la Mungu kwa usahihi wa kina.
2. Kumfanya mtu abadilishwe na neno kiroho na kimwili.
3. Kumfanya mtu aliishi neno kila siku.
4. Kumfanya mtu awe na uwezo binafsi wakupata mahitaji yake kutoka kwa Mungu
kupitia neno la ufunuo.
5. Kumfanya mtu awe na ufahamu pevu kuhusu Mungu wa kweli anemwabudu na
kumtumikia.
6. Kumfanya mtu kuwa na uwezo binafsi wakuishi bila kuathiriwa na mwovu
wakipepo chini ya jua.
7. Kumfanya mtu awe tayari mda wowote kusikia parapanda ya unyakuo.
8. Kumfanya mtu kutembea katika uokovu wa kweli.
9. Kuandaa watumishi na kuwatuma sehemu mbalimbali kwa kazi ya Mungu.
10. Huduma za Maombezi kufungua watu kutoka vifungo vya milango ya kuzimu,
kuponya magonjwa , kufungulia watu milango yakupata kazi n.k.
Mambo hayo kumi, yamekuwa halisi kwa baadhi ya watu wachache waliokubali kujiunga na huduma ya Neno La Ufunuo.