KITABU KITABU KITABU CHA AJABU CHATOKA

Kitabu kilicho sadikiwa kuwa kitabu cha ajabu kimetoka na kutangazwa rasmi na Apostle Alam J. Kayengela jana ijumapili kwenye sherehe za ibada za kustarehe pamoja na Mungu siku ya saba ya ijumapili iliyo barikiwa na Mungu. Niki tabu cha aina yake chenye kurasa zaidi ya 200 kama unavyo kiona hapa kitabu hiki kimekusudiwa kuwafikia wote wenye njaa na kiu ya haki-ambao Bwana Yesu alisema,wanaheri. SIRI YA KUSOMA VITABU VILIVYO ANDIKWA NA ROHO MTAKATIFU -Apostle Kayengela alianza kwa kuelezea kwa ufupi kuhusu kusoma vitabu AKASEMA -Kwamjibu wa Isaya 11;2 Usomaji wa vitabu vyenye uvuvio wa Roho mtakatifu unaruhusu Roho ya maalifa na ufahamu kuja kwako. Ikumbukwe kwamba,watu wa Mungu wana angamizwa kwa kukosa kuwa na maalifa-Hosea 4;6 APOSTLE ALIENDELEA KWA KUSEMA- Unapo soma katika Danieli 9;2 unagundua kwamba, Danieli kwa kuvisma vitabu alipata ufahamu-yaani alipata kujua kitu furani Danieli 1;17 Danieli alipevuka sana kwenye mambo ya ulimwengu wa roho mpaka kujua ...