SIYO LAZIMA UJIKWAE

Ninapo fundisha kwamba HILO SIYO JARIBU, ninakuwa ninamaanisha kabisa toka moyoni mwangu nikitarajia kwamba fundisho hili hutalichukulia kawaida wala hutalipokea kwa uelekevu wa juu juu "Nami nadhani yakuwa MIMI NAMI NINA ROHO WA MUNGU (1Kor 7:40 b) " Yeye aliye na sikio NA ALISIKIE NENO HILI ambalo Roho ayambia makanisa(Uf 2:7) Neno la HILO SIYO JARIBU ulifuatilie vizuri na kulikumbatia maisha yako yote hatimaye utagundua kwamba, Neno hilo limetumwa maalumu kwa ajili yako peke yako na endapo unaamini juu ya MUNGU KUONGEA KUPITIA MAMBO YALIYO ANDIKWA basi utagundua kwamba, NDANI YA HILO SIYO JARIBU kuna sauti ya Mungu ikitembea juu yako MAMBO 4 YENYE NGUVU YANAYO KUSAIDIA KUSHINDA WIMBI LA KUKWAZIKA 1. KUSHINDA WIMBI LA KUKWAZIKA Endapo hujashinda wimbi la kukwazika inamaanisha utakuwa muhanga wa kuchukuliwa kila siku na hilo wimbi, kwasababu inaonekana kila siku wimbi hilo kwa namna moja au nyingine linatumwa katikati yetu ili kutuibia furaha na changamko.