MFULULIZO WA MAFUNDISHO YA APOSTLE ALAM J. KAYENGELA KWENYE KONGAMANO LA SIKU NANE ARUSHA TANZANIA (TAREHE 5-12 MWAKA 2013)
SIKU YA 4:
·
MIUNGU YA YEZEBELI NA
KIZAZI HIKI.
-
Yezebeli
alizaliwa katika familia ya waabudu miungu, wasiomuabudu BWANA MUNGU ALIYEHAI.
Baba yake aliitwa Ethbaal ambaye alikuwa Mfalme wa Sidoni. Yezebeli alikuwa na
muunga niko wa kishetani tokea akiwa kwa baba yake. Ethbaal babayake Yezebeli
kama jina lake lilivyo, alikuwa moja kwa moja amejiunganisha na milango ya
kuzimu – hata jina lake akaliunganisha na miungu aliyoiabudu na kuitumikia.
Alikuwa mchawi na mshirikina wa viwango. Baada ya miaka 38 ya utawala wa Mfalme
Asa, katka Israel – Ahabu alichukua kiti cha ufalme. Ahabu alitafuta mke na
kumuoa Yezebeli binti wa Ethbaal aliyekuwamchawi namwenye ibada bandia za
kishetani – Ifalme 16:29 – 31.
-
Yezebeli
katika kiwango cha uchawi alichokuwa amekifikia, alipewa heshima na shetani
kuwa kama malkia wa kuzimu katika mamlaka ya giza. Alikuwa mzinzi na mwenye
uchawi mwingi sana – 2 Falme 9:22. Yezebeli kwa hila kubwa ya kichawi, alijiita
nabii wa Mungu na kwa utambulisho huo akafanikiwa kuwaangusha wana wa Israeli
na watumishi wengi wengi wa Mungu kwenye uzinzi – Ufunuo 2:20.
Yezebeli
ndiye aliyemuongoza mume wake katika kila jmabo, uchawi aliokuwa nao ulimeza
maamuzi ya Ahabu mume wake. Yezebeli aliendesha oparesheni za kuwaoa na
kuwachinja manabii wa Bwana – 1Falme 18:4 lengo lake ilikuwa kulisambaza lile
giza la uovu katika nchi yote ya Israeli Mts 19 Yezebeli alikuwa na mtandao
mkubwa wa miungu aliyoitumikia na kuimiliki – ukisoma katika 1Falme 18:19
miungu ya baal miungu ya Ashera na muingu ya baal – peori – Hes. 25: 1 – 3 n.k.
Mtandao huo ulimfanya kuwa mwanamke hatari katika ulimwengu waroho na mwili.
Jamii ili muogopa na kumuhofu, alichokiamua ndicho alitenda,na ndicho kilicho
tendeka.
·
Utajuaje una roho za miungu ya
Yezebeli?
-
Tafakari
vizuri 2 Wafalme 9:30 na Yer 4;30 “………..Yezebeli akapata habari, akatia wanja
machoni pake, akapamba kichwa chake……….. ujapo jivika mavazi mekundu, ujapo
jipamba mapambo ya dhahabu, ujapojitia wanja machoni, unajifanya kuwa mzuri
bure tu ……..”
1.
Kutaka
kumuongoza mume wako
2.
Kuvaa
mavazi ambayo aina ya mshono au fasheni yake imewekwa wakfu kwa miungu
3.
Kupaka
wanja – nyusi, mdomo n.k.
4.
Kuvaa
nywele za bandia
Kila anayeshawishiwa
na vitu hivyo bila kujali yeye ni nani – bado hajaepuka miungu ya Yezebeli.
Tabia za miungu ya Yezebeli sasa zimejieneza na kuonekana kusonga mbele hata
kwenye nyumba ya Mungu.
Wanaofuata nyayo za
Yezebeli kwa makusudi – ni wengi, lakini pia wanaofuata tabia za kiyezebeli
pasipo wao kujua wala kukusudia – ni wengi.
-
Utajuaje
kwamba unafuata tabia za Yezebeli kwa makusudi? -Ukionywa ili uache hiyo tabia
unakaidi na kukasirika, kama vile vile Yezebeli alivyokuwa anafanya.
Alimkasirikia mtu yeyote aliyejaribu kumkosoa.
-
Utajuaje
kwamba unafuata roho za miungu ya Yezebeli pasipo kujua wala kukusudia?
Ukionywa tu juu ya tabia hizo za kiyezebeli mara moja unaacha. Ni rahisi tu,
kama hivyo.
·
Kifo cha mtu anayeandama miungu ya
roho ya Yezebeli.
Angalia 2 Wafalme 9:
30 – 37
1. Kwanza unakuwa mwanamke uliyelaaniwa
kwa sababu ya tabia hizo za roho za miungu ya Yezebeli – Mst 34
2. Unakufa kifo cha aibu – Mst 33 – 36 na
unaweza ukafa kifo cha kumwagika damu si kwa sababu una dhambi zingine “Hapana”
bali ni kwa vile unavyoandama roho za miungu ya Yezebeli kwa tabia zake unazo
zipendelea.
3. Kifo chako hakitawasikitisha watu
wengi isipokuwa husema – bora ameondoka.
MAOMBI:
1. Mungu Baba mwenye pendo, nakupenda,
nakupenda, nakupenda sana. Naam Bwana Yesu wewe ni zaidi, unanipenda kupita
upeo. Nisamehe kwani kuna wakati nimekuwa nikiandama roho za miungu ya
Yezebeli.
2. Kila roho ya Yezebeli inayonijia
usingizini kama nyokaleo, Roho mtakatifu anaipiga radi toka mbinguni – kwa jina
laYesu Kristo.
3. Roho za miungu ya Yezebeli na kupiga
stop. Koma kunifuatilia. Simama hapo hapo ulipo na ugande kama friji – Kwa jina
la Yesu Kristo.
4. Mawe yamoto kutoka mbinguni shusha
kipigo kwa miungu ya kiyezebeli inayo niondo lea heshima ya kiMungu maishani
mwangu-Katika Jina la Yesu Kristo
5. Sura yangu, mwili, wangu, nguo
zangu, kataa kushirikiana na roho za miungu ya Yezebeli – katika Jina la Yesu
Kristo.
ZINGATIA
MAELEZO HAYA:
1.
Kama
bado unasikia moyoni mwako kueendelea kushirikiana na bidhaa za Yezebeli ambazo
zimebeba miungu ya Yezebeli – mfano – kupaka wanja, kupaka rangi kwenye kucha
na kupendelea nywele za bandia, ``` kiasi kwamba unaona ugumu kuviacha vitu hivyo
– chukua siku 3 mfululizo ufanye maombi ya kuchoma kwa moto bidhaa za miungu ya
Yezebeli zilizoko ndani yako.
2.
Wakati
mwingine tunalazimika kuviacha vile tunavyo vipenda ilimradi tu, havimletei Mungu
heshima. Chochote ambacho Mungu hajaturuhusu kwenye neno lake siyo chetu, bali
ni vya ulimwengu.
3.
Bila
kujali utaonekanaje katika jamii inayokuzunguka, unalazimika kumsikiliza Roho
mtakatifu anayekusihi kwa sauti ya upendo ili uachane kabisa na namna yoyote ya
kiyezebeli, ambayo kwa muda mrefu – imekupunguzia uwepo wa Mungu.
v ONYO!!!
Umekatazwa kutoa copy ujumbe ulioko
kwenye karatasi hii ili kumpa mwingine,isipokuwa umeruhusiwa kumchukulia rafiki
yako karatasi yake mwenyewe. Itakuwa dhambi ya makusudi ya kutokutii usipo
zingatia onyo hili.
AMINA!!!!.
Comments
Post a Comment