NENO LA UFUNUO LA WIKI HII KWA KANISA ULIMWENGUNI-Sehemu ya 3 MATOKEO YA UGONJWA WA USAHAULIFU

Msahaulifu kamwe hakuwahi kujua matokeo ya ugonjwa ule alio ambiwa na Dkt. wake [ugonjwa wa usahaulifu] KUSOMA SHULE NZURI BILA MAFANIKIO Msahaulifu alikuja kugundua ugonjwa wake wa usahaulifu ulivyo mbaya baada ya kutumia miaka mikgi sana shuleni bila mafanikio. KUFERI KILA MTIHANI DARASANI Sikumoja msahaulifu alimwita mwalimu wake pembeni,huku akiwa amenyongonyea sana na kumuuliza- Mwalimu,mimi mbona kila mtihani nimekuwa nikiferi? au labda wachawi wananisumbua?kwanini naferi kila mtihani? Mwalimu wakati anamjibu,alimkazia macho akamnyoshea fimbo nakumwambia- Unakumbuka nimekuwa nikikuuliza uniambie ulicho jifunza unaniambia nimesahau? sasa kama unasahau ninacho kufundisha,unategemea kushinda mtihani?- kwasababu pia msahaulifu hakuwa na muda wa kutembelea daftali zake ili kujisomea yale aliyo jifunza. Mwalimu alisikitika sana akamwambia- SASA ONA,hata mitihani midogo inakushinda ...