NENOLAUFUNUO KWAKANISA ULIMWENGUNI-sehemu ya pili-MFANO WA MTU ANAYE ITWA MSAHAULIFU
Mwalimu na Mtume Aram J.Kayengela kiongozi mkuu mwanzirishi wa Huduma ya Neno la Ufunuo yenye makao makuu Dar es salaam Tnzania Manispaa ya Ilala Kata ya Chanika-Jana alikuwa akiendeleza ujumbe wa wiki iliyo pita. Akasema;
LEO NITAKUWA NAONGELEA MFANO WA MTU ANAYEITWA MSAHAULIFU
a
Alielezea kwamfano halisi kuhusu mtu aitwaye msahaulifu jinsi alivyo zaliwa. Akasema,
Mtu huyu aitwaye msahaulifu alizaliwa nababa mwenye uwezo. Uwezo wa kiakili,kipesa,n.k
Kulingana na mazingira aliyo zaliwa mtu huyu aitwaye msahaulifu yalivyo kuwa yakiuwezo,alipelekwa shule nzuri sana,shule yenye mafunzo yasiyo patikana kwa urahisi.
Malezi yamtuhuyu(msahaulifu) yalikuwa yaghalama sana,kwani baba yake alimuandalia malezi mzuri sana aliye mlisha chakula bora kilicho pimwa.
Katika upande wa matatizo ya kiafya-mzazi wake alihakikisha huyu msahaulifu anachekiwa kilamwezi,katika hali ya kawaida kwakweli msahaulifu huyu hakuwahi kukutwa na tatizo lolote kama TB,KISUKALI,HOMA,KANSA,UVIMBE,WALA UKIMWI-kwasababu hata hivyo alikuwa amesha mkatia BIMA YA AFYA-alikuwa amedhaminiwa kwa habali ya matibabu-kwamfano wake kama yule mtu aliyeangukia mikononi mwa wanyanganyi alipata mtu aliye mkatia bima ya afya nakumwambia mwenye hospili kwamba,ghalama yote ya matibabu atalipa yeye-taz Luka 10;25-35
Mwanzo wa matatizo mabaya ya mtu huyu aliyepewa jina la msahaulifu;
Siku moja msahaulifu alitoka nyumbani akaenda kutembea na kuangalia manzari ya mji,karibu kila mahali alipo pita kulikuwa nashamra shamra zamji hivyo naye alikuwa anashawishika nakuingia kwenye shamra shamra hizo-sasa hakuwa ameelewa kwamba,wale wote walio kuwa kwenye stalehe zile,kuna wakati mdudu furani mwenye tumbo kubwa nakichwa chembamba,huwa anakuja kuwa n'gata,kwahiyo na msahaulifu naye akawa amen'gatwa nayule mdudu,na sumu ya ugonjwa ikamwingia-alipopimwa na Dkt.-Dakitari akamwambia"pole sana umepatwa na ugonjwa mbaya sana" msahaulifu akiwa ametoa jicho kubwa alipayuka nakuuliza,UGONJWA GANI?
Dkt. kwahuruma,akamwambia-yulemdudu aliyekun'gata aliingiza ndani yako sumu ya ugonjwa wa ajabusana-msahaulifu akauliza tena kwa mkazo NIUGONJWA GANI?-dkt akamwambia,ugonjwa huo unaitwa"UGONJWA WA USAHAULIFU" msahaulifu alipo sikia jibu hilo,alicheka kidogo akasema"sawa"nilifikiri nimepatwa na tatizo kubwa-akaendazake,yeye hakuwa ameelewa kwamba ugonjwa wa usahaulifu nimbaya sana mpaka baadaye alipo anza kuona matokeo ya huu ugonjwa(itaendelea)
Baba yake msahaulifu ilibidi aanze juhudi za kumsaidia mwanae,kwani alijua fika kwamba,mwanae amesha patikana naugonjwa mbaya sana kuliko hata ukimwi.
Huduma yake ya kwanza katika kumsaidia,ilibidi ampige marufuku kwenda huko kwenye miji ya starehe-kwani alijua habari ya yule mdudu
Huduma ya pili,Alimpa dawa ya kumeza kila siku-akilenga kushughulikia ile sumu
Huduma ya tatu,Alimletea mtu wa karibu sana-kwasherti kwamba mshaulifu atapaswa kumsemesha huyo mtu kila siku,asipo msemesha yeye hatafanya chochote hata kama ameletwa kwa lengo la kumsaidia huyu msahaulifu.
kisha Apostle Kayengela akasema,
YESU ANA KUFUNDISHA NINI KATIKA UFUNUO ULIOKO NDANI YA MFANO HUU?
Akasema,
MAANA YA MFANO HUU NIKWAMBA;
Msahaulifu aliye tajwa hapa,nimlokole aliye zaliwa mara ya pili kama 1pet 1;23 inavyo eleza.
-Nimtu ambaye anaacha kutimiza yampasayo kwakuwa yamempoea(amesahau)
Shule yenye mafunzo mazuri aliyo soma msahaulifu yenye mafunzo yasiyo patikana kwa urahisi-ni lile Neno la Ufunuo unalo shirikishwa hapa-huwa halipatikani kwa urahisi
Mithali 4;2 anasema "Nawapa mafundisho mazuri....."
-Ukweli nikwamba,Huduma ya Neno la Ufunuo nimoja ya Huduma zenye mafundisho mazuri ya kiufunuo Duniani-ndoile shule aliyo soma msahaulifu(katika mfano wetu)
Mathayo 15;9 Yesu alisema kuhusu mafalisayo"watu hawa hufundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu..."-Unahatali kubwa kama katika kanisa lako unapokea mafundisho yanamna hii yaliyo maagizo ya wanadamu.Hutafika kokote kiroho.Makanisa mengi hawafundishwi Neno la ufunuo linalo toka kwa Mungu moja kwa moja,bali hutunga njumbe kwa hisia zao yaani maagizo yaliyo ya wanadamu,na hayo humfifisha tu mtu kiroho.
Yoh 7;15 Yesu alisema,mafunzo aliyo fundisha alikuwa akifunuliwa moja kwa moja.Hakutunga somo bila kufunuliwa,ndiyo maana mahubiri yake yalikuwa ya kiufunuo
Vile msahaulifu alivyo chekiwa kila mara nakupewa bima ya afya hii ndo-Isaya 53;4-5 na mathayo 8;17 (Hakika aliyachukua magonjwa yetu na kujitwika fadhaa zetu na kwa kupigwa kwake sisi tumepona)Hii ni bima ya afya waliyo katiwa walokole kama wakijua hilo.Hupaswi kuugua ikiwa Yesu amesha lipia.Kma una shindwa kupokea uonyaji hebu tafuta kwa bidii Neno la Ufunuo,siyo maombezi tu.
Malezi ya gharama na mlezi mzuri aliyemlisha chakula bora msahaulifu-kwamjibu wa Yoh 21;15 Yesu alimwambia Petro"LISHA WANA KONDOO WANGU" Petro alipewa kazi ya kulisha. Hivyo tuna weza kusema,yule aliye tumwa na Mungu kuku lisha wewe Neno zuri ndo yule mlezi tuliye muona pale.Katika Yer 3;15 anasema Mngu-Nami nita wapa wachungaji wanipendezao moyo watakao walisha kwa malifa nafahamu. hata Ez 34;14
Msahaulifu kwenda mjini kwenye starehe nivile ambavyo huwa unaruhusu mawazo yako yatembee kwa kufikiri zaidi mambo ya duniani-1Yoh 2;15-umekatazwa hilo.Ndiyo maana katika Wakolosai 3;2 anasema,uyafikiri tu,mambo yajuu(yambinguni)siyo ya duniani.
-Yule mdudu mwenye sumu aliye natumbo kubwa kichwa kidogo-hizo ndizo starehe hasa zadunia. Ukiziwaza sana huta kumbuka chochote cha Ufalme wa Mungu.
Alipo pimwa na kuambiwa anatatizo baya laugonjwa wa kusahau hakushituka,hivi hasa ndivyo watu wanavyo chukulia kawaida tatizo hili la kusahau,japo wengi wametangulia kuzimu nawengi wataenda kwa tatizo hili hili"la ugonjwa wa kusahau"
-Watu wako tayali kumlilia Mungu awape mke mwema,au watoto au mtaji mkubwa au uponyaji,lakini siyo ushirika na Roho mtakatifu wa kuwa kumbusha mambo.
Zile huduma tatu za mzazi wake alizo chukua ili kumsaidia
Huduma ya kwanza
Kwanza ikumbukwe kabisa kwamba mzazi huyu anaye zungumzwa hapa ni Mungu mwenyewe anaye fanya juhudi ya kuku kumbusha ili uwe na urafiki na Roho mtakatifu atakaye kuku mbusha
Huduma ya pili
-Alimpiga marufuku kwenda kule kwenye starehe-maanayake Mungu hataki utumie muda wako mwingi kupeleka mawazo yako kwenye mambo ya dunia,kama nilivyo sema hapo mwazo.
Huduma ya tatu
-Alimletea mtu wa karibu sana-Huyu ndiye Roho mtakatifu tuliye letewa,yeye hakusemeshi usipo msemesha,hakukumbushi usipo mwambia nikumbushe.Atakuwepo tu hapo.Katika yohana 14;26"...Atawakumbusha YOTE.." HUYO TU,NDIYE ANAYE WEZA KUONDOA UGONJWA wote WA KUSAHAU.
NAMNA YA KUKU MBUSHWA NA ROHO MTAKATIFU
Soma vizuri kwanza Tito 3;1-2 kisha tamka maneno ya mfano huu
1.Roho mtakatifu naomba leo unikumbushe kunyenye kea kwa kiongozi wangu-kazini kanisani n.k
2.Naomba leo unikumbushe kutii Neno lako
3.Naomba leo unikumbushe kuwa tayali kwa kazi ya Huduma-nikumbushe kusapoti kazi yako
4.Naomba unikumbushe leo kulinda kinywa changu kisitoe matusi
5.Naomba Roho mtakatifu leo unikumbushe kuonyesha upole kwa watu wote
6.Nikumbushe nata leo niamke usiku saa 8 kumuombea Apostle Kayengela ili namimi nishiriki mafuta na neema nyingi ulizo mkirimia
7.Naomba Roho mtakatifu leo unikumbushe kuwahi ibada
8.Naomba,unikumbushe kulipa zaka na dhabihu kwa uaminifu bila kinyongo
MWISHO OMBA OMBI HILI
ROHOMTAKATIFU ONDOA NDANI YANGU UGONJWA WA USAHAULIFU. HARIBU KABISA UGONJWA WA USAHAULIFU NDANI YANGU.ANGAMIZA KABISA SUMU YOTE YA USAHAULIFU NDANI YANGU.
SASA ANZA KUPIGA MAKOFI NAKUMSHUKURU MUNGU KWA NENO LAKE LA UFUNUO AMBALO AMEKUWA ANAKULETEA KUPITIA MTUMISHIWAKE ARAM J.KAYENGELA
AMINA
Comments
Post a Comment