NENO LA UFUNUO LA WIKI HII KWA KANISA ULIMWENGUNI-Sehemu ya 3 MATOKEO YA UGONJWA WA USAHAULIFU
Msahaulifu kamwe hakuwahi kujua matokeo ya ugonjwa ule alio ambiwa na Dkt. wake [ugonjwa wa usahaulifu]
KUSOMA SHULE NZURI BILA MAFANIKIO
Msahaulifu alikuja kugundua ugonjwa wake wa usahaulifu ulivyo mbaya baada ya kutumia miaka mikgi sana shuleni bila mafanikio.
KUFERI KILA MTIHANI DARASANI
Sikumoja msahaulifu alimwita mwalimu wake pembeni,huku akiwa amenyongonyea sana na kumuuliza-Mwalimu,mimi mbona kila mtihani nimekuwa nikiferi? au labda wachawi wananisumbua?kwanini naferi kila mtihani?
Mwalimu wakati anamjibu,alimkazia macho akamnyoshea fimbo nakumwambia-Unakumbuka nimekuwa nikikuuliza uniambie ulicho jifunza unaniambia nimesahau? sasa kama unasahau ninacho kufundisha,unategemea kushinda mtihani?-kwasababu pia msahaulifu hakuwa na muda wa kutembelea daftali zake ili kujisomea yale aliyo jifunza.
Mwalimu alisikitika sana akamwambia-SASA ONA,hata mitihani midogo inakushinda
<itaendelea>
MAANA YA UFUNUO HUU
1.MIAKA MINGI SHULENI BILA MAFANIKIO
Niyule anaye weza kukaa kanisani miaka mingi bila kuona mafanikio kwasababu ya kuendelea kuendekeza ugonjwa huu wa usahaulifu. Ndiyo maana Mungu anaonya katika Yoshua 1;8-yatafakari maneno yake mchana na usiku
Na katika Mith 3;1-usisahau sheria yangu
pia katika 1timotheo 4;13,15 -ufanye bidii katika kusoma....."
-Mungu anacho sisitiza hapa,nikwamba hataki kabisa uwe na ugonjwa huu wa kusahau.Hataki usahau yale unayo jifunza kwasababu nihatali sana.
Kumbuka"msahaulifu alikaa kwenye shule ya viwango miaka mingi bila kuona mafanikio-kwasababu hakuwa na tabia ya kujisomea yale aliyo yaandika kwenye daftali yake,hivyo AKAWA ANASAHAU.
2.MSAHAULIFU KUFERI KILA MTIHANI DARASANI
Hii inamaanisha kwamba,unapokuwa unasahau yale ambayo Mungu anakufundisha humanisha kuwa,utashindwa pale jaribu litakapo kujia. maana majaribu ndo mitihani yakiroho. Jaribu lita kutetelesha na kuku changanya ikiwa utakuwa mwepesi wa kusahau kile ufundishwacho na Mungu.Majaribu yatakuchanganya sana kama utakuwa muathirika wa ugonjwa huu mbaya wa usahaulifu.
Unafahamu kuwa Mungu ndiye akufundishaye? japo kuwa hapo ulipo humuoni,lakini yuko kazini kuku fundisha.
-Mithali 4;2 "nawapa mafundisho mazuri ili msiiache sheria yangu
- Zab 32;8 "Nitakufundisha nakuku onyesha njia utakayo iendea"
-Isaya 48;17"Mimi ni Bwana Mungu wako nikufundishaye ili upate faida...."
-Kwanini watu wengi wanaferi mitihani ya majaribu? nikwasababu wamepatikana na ugonjwa mbaya wa kusahau kile walicho fundishwa na Mungu. Nawengine huwa hawajui kama kweli ni Mungu anaye wafundisha.
MSAHAULIFU ALIANGUSHWA NA MITIHANI MIDOGO SANA DARASANI
Mitihani hii huwa nimajaribu ambayo Mungu huyaruhusu yakufikie
Kumbu kumbu 8;3"....akakuacha uone njaa.."
-Ona. Huwa kunawakati anaamua kuku acha upitie jambo furani la kimaumivu.Hapo ndipo anataka ukumbuke kile alicho kufundisha. Hawezi kuku letea mtihani ambao hajakufundisha somo lake.
-2nyakati 32;31"...Mungu akamuacha ili amjaribu...."
Wengine hufikiri kwamba Mungu hawezi kuwajaribu. Basi atakuwa siyo mwalimu. Anapo kufundisha lazima siku moja utafanyia mtihani hayo mafunzo. Msahaulifu hakuwa anajali hilo.
-Mitihani midogo iliyo mshinda msahaulifu-ndo yale majaribu madogo tu,ambayo huwaangusha watakatifu wengi lakini tatizo kubwa ni ule ugonjwa wa usahaulifu.
OMBA OMBI HILI
Ee Mungu uliye hai,nimetambua kwamba wewe ndio unaye nifundisha ili nipate faida,nakataa ugonja huu wa usahaulifu,kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazaleth.
maombezi
AMINA
KWAMSAADA ZAIDI WASIRIANA NASI KWA;
mlkayengela@gmail.com
alamkayengela@yahoo.com
0763359745 na 0712583194
Comments
Post a Comment