NENO LA UFUNUO LA WIKI HII KWA KANISA ULIMWENGUNI - SEHEMU YA 5

TUNZA KICHEKO CHA MOYONI. Mtume Alam Kayengela akiwahudumia waamini waliofika katika ibada jumapili hii. Mwanzo 17:15 - 19 Mst 17 "Ndipo Ibrahimu akaanguka kifudifudi, akacheka akasema moyoni , Je mtu wa umri wa miaka mia kwake atazaliwa mtoto? Mwanzo 18:12 " Kwahiyo Sara akacheka moyoni mwake, akasema niwapo mkongwe nitapata furaha na bwana wangu mzee? Mtume Alam Kayengela akimuhudumia muumini aliyefika katika ibada jumapili hii. ANGALIA HILO: "Kwahiyo Sara akacheka moyoni mwake. Lakini akilini mwake alikuwa na kilio cha bibi kizee, mkongwe asiye weza kubeba mimba. Akacheka moyoni pale NENO lilipo mjia. Kutunza kicheko cha moyoni inamaanisha kutunza furaha ya moyoni. Kukosa furaha nisawa na kuwa mateka, unapokosa furaha wewe ni mfungwa, asiye huru. Umefungwa na nini? Mfano: kama umepata hasara fulani ikaupelekea kukosa furaha maana yake hiyo hasara imefanyika mnyororo wa kukufunga ili usipate furaha......... Itaendelea wiki ij...