WIKI HII-Kazana na kuilinda Enzi yako
NDIYO,KAZANA NA KUILINDA ENZI YAKO
Hayo yalisemwa na kiongozi mkuu mwanzirishi wa Huduma ya Neno la ufunuo Tanzania,alipo kuwa anaongea na Watumishi wa Mungu watenda kazi wa Huduma hiyo jijini Dar es salaam-Chanika. Mtume Aram J.Kayengela alianza kwa kusoma kitabu cha Yuda 1;6 akasema-Malaika walio shindwa kuilinda enzi yao,nakuacha kuyalinda vema makao yaliyo wahusu,walitupwa pamoja na shetani kwenye vifungo vya giza mpaka leo. Toba yao haitakubalika mpaka milele.
Mtume Kayengela,alifafanua maana ya enzi nakusema kuwa;
ENZI NI;
1.Nafasi muhimu uliyo pewa-yaweza kuwa nafasi ya cheo,n.k
2.Enzi ni heshima unayo pewa
3.Enzi ni upendeleo(kupata kitu ambacho wengine wanakitamani ila hawakipat) yaweza kuwa hata nafasi ya cheo chako au vinginevyo
4.Enzi ni Baraka-unajua baraka humfikisha mtu mahali pa enzi.
5.Mfano rahisi wa enzi nikama nafasi ya kuajiriwa. Unabosi wako juu yako
6.Enzi ni kibari cha kuingia mahali(fursa)
UNAILINDAJE ENZI YAKO?
Nikwakujiwekea alama zanjia,yaani kuiruhusu nakuilazimisha akili yako kutembelea yale yote uliyo pitia,kama mapito ya majaribu-kumbu kumbu la torati 8;2 na mst wa 10-14
-Mtume Kayengela alisema,Mungu aliwasisitiza wana wa Israel wajihadhari sana wasije wakasahau mapito waliyo pitia kwa msaada wake wakavuka.Hajabadirika mpaka sasa ana ongea na wewe kuku kumbusha "JIHADHARI USIJE UKASAHAU MAJARIBU NILIYO KUVUSHA"
Kayengela alisema kwamba,kuna watu hawakumbuki kwamba kuna wakati walikuwa hawana kazi,au walikuwa hawana nafasi walizo nazo leo, wengine hawakumbuki kwamba kuna wakati walikuwa hawna hata uwezo wa kujenga nyumba zao wenyewe. Umesahau kwamba kuna wakati ulikuwa hata kitanda huna.Kwakuwa hayo huwa huna muda wa kuya fikiria,ndiyomaana tunapo kwambia leo uwezeshe huduma hii kipesa unaona kama vile umeambiwa kwa muda usio sahihi.Pengine utasema,hilo siyo kanisa langu,nita mtolea Mungu kanisani kwangu.Chunguza sana fikra yako hiyo. Usije ukamfanya Mungu ajute kwa sababu amekufikisha hapo ulipo leo. Yesu alisema,kondoo wangu waisikia sauti yangu.Kondoo amesha elewa kinacho maanishwa hapa. Kondoo amesha elewa Mungu anacho ongea hapa.
MIFANO HALISI YA WALIO SHINDWA KULINDA ENZI ZAO
1.Malaika waasi walio mskiliza muasi shetani-walittupwa pamoja naye. Leo wanaitwa pepo wachafu
2.Mfalme Sauli- 1samweli 10..................
3.Lusifa-kutoka kuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta nakuwa shetani-ezk 28 na isaya 14
4.Mtu wa Mungu nabii kijana-1Falme 13
5.Anania na mkewe-Matendo 5
6.Yuda iskali yote-kutoka kuwa mtume,kisha kuwa msaliti wa Damu isiyo na hatia-math 27
7.Akani-yoshua 6-7
8.Gehazi-kutoka kuwa mchungaji msaidizi,nakuwa mrithi wa ukoma-2Falme 5
9.Wabarikiwa wanao jiondoa kwenye asiri ya uzima wao(kusudi)
SABABU ZA KUSHINDWA KULINDA ENZI YAKO
1.Malaika waasi sababu yao ilikuwa kusikiliza mwovu aliye asi.
2.Sauli-sababu ilikuwa kukosa utii
3.Lusifa-sababu ilikuwa kiburi cha uzuri
4.Mtu wa Mungu nabii kijana-sababu ilikuwa kuto kushika au kuzingatia maelekezo muhimu
5.Anania na mkewe-sababu ilikuwa roho ya kumpunguzia hadhi Mungu,hii ndo roho ya kaini ya kumpa Mungu vitu vya hadhi ya chini lakini vyakwake vinakuwa vya hadhi
6.Yuda skali yote-sababu ilikuwa kupenda sana hela. Inaitwa roho ya urafi wa fedha
7.Akani-sababu ilikuwa wizi wa kiroho
8.Gehazi-sababu ilikuwa kukosa uaminifu wa sirini-alifikiri kiongozi wake hamuoni kwa tendo lile alilo fanya sirini.
9.Wabarikiwa-sababu nikuangalia sana mazingira ya sasa bila kuwekea mkazo mambo ya usoni
Barikiwa sana msomaji wangu. Nakupenda
Karibu kwenye Huduma ya Neno la Ufunuo-Chanika mtaa wa kaanani lukooni karibu na shule ya msingi
AMINA
Comments
Post a Comment