NENO LA UFUNUO LA WIKI HII-Jinsi Neno la Ufunuo linavyo husika kuyafumbua macho yako
Luka 24;31 “Yakafumbuliwa macho yao wakamtambua; kisha
akatoweka mbele yao”.
Macho yako yanapofumbuliwa ndipo unapomtambua Yesu. Macho
yanayozungumzwa hapa siyo haya ya kawaida. Macho haya ya kawaida yamenajisiwa
na vitu vingi kiasi kwamba Mungu hapendi kuyaruhusu yamwone (Ndio maana Mungu
hujificha sana)
Mara nyingi watu waliofungwa na roho hii chafu ya kutaka
kumwona Mungu kwa macho haya ya kawaida, ni wale waliotoka kwenye framilia ya
Tomaso (wa kizazi kisichosadiki bila kuona).
NI MACHO GANI HASA YAFUMBULIWE KWANGU ILI NIMWONE MUNGU KILA
MARA?
Efeso 1:18 “Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru,………….” Ni macho
ya moyo wangu. Yanapotiwa nuru na Neno la Ufunuo ndipo yanapofumbuka- Zaburi
119:130 “Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, na kumfahamisha mjinga”
Sikuzote ifahamike ya kwamba Neno la Ufunuo ni lile
lililofafanuliwa kiufunuo.
SABABU KUBWA INAYOSABABISHA MARA KWA MARA WEWE KUTOMWONA
MUNGU
Hiyo sababu utaijua leo na kufumbuliwa macho yako. Si wengi
wanaojua sababu inayosababisha mara kwa mara wasimwone Mungu.
Sababu hiyo ni kwamba, hujajua kumtazama Mungu kwa macho ya
moyo. Wengi hawajui kama moyo una macho.
MACHO YA MOYO NI NINI?
Jibu ni rahisi- Macho ya moyo ni hisia takatifu maana yake
unapokuwa kwenye maombi unamhisi Mungu kuwepo hapo ulipo saa hiyohiyo au muda
huohuo. Hutahisi kuwa Mungu yuko mbali utahisi ukaribu wake kwako.
Macho ya moyoni ni fikra takatifu unayoiruhusu kumwona Mungu
kwa kila jambo- Wakolosai 3:23 “Lolote mfanyalo, fanyeni kwa moyo, kama kwa
Bwana, wala si kwa wanadamu”.
Maana yake hata unaposoma ujumbe huu hisia yako takatifu
inaweza ikahisi uwepo wa Mungu akikufundisha.
Ninapotoa sadaka kwa ajili ya kusudi la Mungu na siyo kwa
manufaa yangu tu kwa urahisi naelewa nafanya kwa Bwana. Kumbuka macho yako(macho
ya moyo wako) hayatafumbuka bila Neno la Ufunuo.
AMINA!!!!!
Comments
Post a Comment