MFULULIZO WA MAFUNDISHO YA APOSTLE ALAM J. KAYENGELA KWENYE KONGAMANO LA SIKU NANE ARUSHA TANZANIA (TAREHE 5-12 MWAKA 2013)
SIKU YA 8:
·
NAMNA YA KUPOKEA
USHINDI WA MUNGU DHIDI YA MIUNGU.
-
Hii
inamaanisha namna ya kupokea mbinu za kushinda miungu.
-
Misingi
4 ya vyanzo vya nguvu za Mungu inayokufanya upate NGUVU YA MUNGU ya kushinda
miungu migeni ya kipepo.
·
Msingi
wa kwanza: AMUA KUWA SADAKA
Unapofikia maamuzi haya ya kuwa
sadaka ya Mungu siyo rahisi hatakidogo kushindwa na miungu.
·
Kumbuka -
Isaka alikuwa sadaka iliyotolewa kwa
Mungu – Mwz
22:1 – 2. Ukubwani mwake, shetani alijaribu kumuangamiza kwa njaa kali – Mwz 26:1-5,
Isaka alipitia msukosuko kwenye ndoa – Mwz 26:6-11 - bado Isaka alidhulumiwa
visima zaidi ya viwili – Mst 18 – 23. Hayo yote ikiwa ni pamoja nayeye
kucheleweshewa mtoto (uzao – Mwz 25:21) lakini pamoja na hayo yote aliibuka
msindi na akawa mkuu – Mwz26:12-14 sadaka huwa haishindwi na miungu kamwe –
Isaka alikuwa sadaka. Sadaka ya Mungu aliye hai.
·
Kumbuka – Samweli alikuwa sadaka ya Mungu – 1 Samweli 1:11 na Mst 24. Alizaliwa katika kipindi
ambacho miungu ilikuwa imeharibu kabisa hali ya hewa ya kiroho – Neno la Bwana la ufunuo lilikuwa adimu – 3:1 (b)
ni wakati huo ndo miungu ilikuwa imeshika kasi kuendesha oparesheni za hapa na
pale mpaka sanduku la Bwana likawa limechukuliwa – 1 Samweli 5:1-2. Samweli
ukubwani mwake alipitia changamoto nyingi mpaka za kuchaniwa nguo – 1 Samweli
15:27 lakini hata hivyo hakushindwa. Adui si mara moja waliazimia mabaya kwa
Samweli 19:18 – 24. Mpaka walisalimu amri kwa sababu Samweli alikuwa sadaka ya
Mungu – Sadaka haishindwi.
·
Kumbuka – Yesu Kristo alikuwa sadaka
-Yoh 3:16 alianza kuviziwa na miungu iliyokuwa nyuma ya Herode akiwa bado mdogo
tu wa miaka miwili – Math 2:13-18 miungu ya nyikani uso kwa uso ilipambana na
Bwana Yesu bila mafanikio – Math 4:1-11, kwa sababu yeye alikuwa sadaka.
Aliviziwa sana ili angalau aweze kukamatwa hata kwa maneno yake – Luka 20:20,
ikashindikana. Kwa sababu sadaka haishindwi, mwisho Yesu Kristo aliibuka
mshindi na akakiri hivyo – nimeshinda ulimwengu – Yoh 16:33 (b) hakushindwa. Alishinda.
·
Kumbuka pointi hii – ukiamua kuwa sadaka ya Mungu unapata neema ya kupakwa mafuta
ya tofauti – ndivyo Mungu anavyosema
kwenye Zaburi 45:7, Sauli alipakwa mafuta ya chupa – 1 Samweli 10:1 – lakini
Daudi alipakwa mafuta ya Pembe - 1 Samweli 16:13. Pembe inawakilisha nini?
Ukisoma katika ufunuo 17:12 pembe ni ufalme au mamlaka yenye nguvu.
·
Msingi
wa pili: ONGEZA USIKIVU WAKO WA KIROHO NA UWE MTU WA KUTULIA – ndipo utaweza kuishinda miungu.
Miungu hautaishinda kwa maombi tu, “Hapana” msingi huu wa pili wa maisha ya
kiroho, uwe ndo msingi wa maisha yako ya kila siku kuanzia leo. Katika Mwz 1:1-
2 Mungu alipoona matatizo ya ukiwa,
utupu na giza, hakukurupuka kufanya chochote isipokuwa “ALITULIA KWANZA” baada
ya kutulia alijua kipi aanze nacho, na kwa namna gani.
·
Siku ya kwanza – AkawekaNuru – Mst 3-5
·
Siku ya pili – Akaweka Anga (Mbingu) Mst 6-8
·
Siku ya tatu – Akaweka Nchi na bahari – Mst 9-13
·
Siku ya nne – Akaweka Mianga ya majira na nyakati pamoja na nyota – Mst 14-19
·
Siku ya tano – Akaweka Viumbe vya baharini na ndege wa angani – Mst 20 – 23
·
Siku ya sita – Akaweka Wanyama wa kila aina na mwanadamu – Mst 24 -31
·
Siku ya saba – Akastarehe bila kufanya chochote – Mwz 2:1 – Maana yake usifanye kazi
kama roboti Pumzika.
·
Kutulia
ni tabia ya Mungu inayokufanya uwe na mwelekeo wa kufanya vitu sahihi vilivyo
katika mpangilio sahihi.
·
Mfano – Nini kingetokea kama Mungu angeumba
samaki siku ya pili? Kwa maana bahari haikuwepo bado, nini kingetokea kama
angeumba mwanadamu kabla ya Nchi? Maana yake angeishi baharini.
·
Usipokuwa
na muda wa kutulia mbele za Mungu, kimawazo, kishughuli n.k. lazima miungu
itakuchanganya tu, kwa sababu hautakuwa na mwelekeo. Kitu cha kufanya kesho
utakifanya leo, cha leo utakifanya kesho – mahali pa kuweka viatu utaweka mswaki,
mahali pa mswaki utaweka soksi, mahali pa soksi utaweka Biblia, mahali pa
biblia utaweka nguo n.k. Ukitaka kuvaa kiatu, utakitafuta kwanza, kudhihirisha
ujinga ulio nao wa kuweka vitu kwa mpangilio. Kwa namna hiyo miungu huwezi
kuishinda kwa sababu huna mpangilio wala mwelekeo – umekuwa mtu wa kubebanisha
mambo ovyo.
·
Madhara
ya kukosa utulivu hata hayawezi kuvumilika – kwanza hutajua uanze na lipi na umalize na lipi –
zaidi ni kwamba unaandamwa na roho ya kuchelewa au kuchelewesha mambo, utakuwa
mtu wa kuzunguka kila mara kwenye uwanja wa kutafuta vitu ambavyo umesahau
ulipoviweka. Na utakuwa mtu wa kuanza upya kila mara kwa sababu unafanya vitu
kabla ya wakati au kwa kuchelewa.
·
Msingi wa tatu –
KUBALI
MAPENZI YAKO YAVUNJIKE YA MUNGU YASIMAME – huo ndio ulikuwa moyo wa Daudi –
Mungu akapendezwa - Matendo 13:22 kwa
sababu hiyo, Daudi akaishinda miungu – 1 Samweli 17:42-43. Fika hatua mambo
yako yaharibike ya Mungu uyafanikishe.
·
Msingi wa nne – JINYENYEKESHE
ILI UWE NA ROHO ZA MIUNGU WATAKATIFU NDANI YAKO.
-
Unakumbuka
Danieli – kwa sababu ya unyenyekevu, ndani yake ziliachiliwa roho za miungu
watakatatifu toka kwa Mungu – Danieli 5:11 – hizo siyo roho za mapepo, bali ni
Roho 7 za Mungu – Ufunuo 5:6, hizi Roho 7 za Mungu ndo zile zimeorodheshwa
kwenye Isaya 11:2.
-
Kuwa
na Roho za miungu watakatifu ndani yako ni jinsi gani unajitahidi kutafuta
tabia hizo 7 za Mungu ili ziwe maishani mwako.
-
Ukishakuwa
na Roho za miungu watakatifu ndani yako, ndipo unakuwa mungu mdogo chini ya jua
– 1 Samweli 4:8 – walitenda kama miungu. Ndipo Neno la Yoh 10:34 – 35 linatimia
kwako “NDINYI MIUNGU”
·
MAELEKEZO
-
Tafuta
nafasi ya kufanya maombi ya kumwambia Roho mtakatifu akusaidie na kukuweka
kwenye misingi hiyo 4.
v
ONYO!!!
Umekatazwa kutoa copy ujumbe ulioko kwenye karatasi hii ili
kumpa mwingine,isipokuwa umeruhusiwa kumchukulia rafiki yako karatasi yake
mwenyewe. Itakuwa dhambi ya makusudi ya kutokutii usipo zingatia onyo hili.
AMINA!!!!.
Comments
Post a Comment