MFULULIZO WA MAFUNDISHO YA APOSTLE ALAM J. KAYENGELA KWENYE KONGAMANO LA SIKU NANE ARUSHA TANZANIA (TAREHE 5-12 MWAKA 2013)
SIKU YA 5:
·
BAADHI YA AINA ZA MIUNGU YA WAFILISTI NA MIJI YA MADHABAHU ZAO.
1.
Dagoni – tazama, katika Waamuzi 16:23 –
Dagoni alikuwa Mungu wa Wafilisti. Ni moja ya miungu iliyohusika katika harakati
za kumkamata Samsoni – Waamuzi 16:1-31 Hata sasa ziko kazini hizo roho.
2.
Maashtorethi – 1 Samweli 31:8 – 13 – Maashtorethi
ni miungu ya Wafilisti iliyoongoza operesheni za kummaliza Mfalme Sauli.
Zinafanya hivyo hata leo.
3.
Beth – shan – Samweli 31:8-13 – Beth – Shan ni mungu
wa Wafilisti anayeendesha shughuli za kujenga kuta. Ndiye anayejenga kuta hata
nyakati zetu hizi.Kuta za kiroho
4. Baal
– Zebuhu – 2 Falme
1:2 – Baal – Zebubu ni Mungu wa
kigeni wa Wafilist anayetenda kazi kwa ushirika wa karibu na Abadoni au
Apolioni malaika wa kuzimu – Ufunuo 9:11 Baal – Zebubu kwa ushirika wa pamoja
na Apolioni zilikuwa roho zilizoweza kuwavuta hata Wafalme kwenda kwa waganga
wa kienyeji. Baal – Zebubu katika Agano jipya alitambulika kama – beel zebuli
mkuu wa mapepo – Math 12:22 – 24.
5. Baal
– peori – Hesabu
25:1-3 baal – peori ni mungu wa wafilisti aliyeongoza harakati za kuwaunganisha
wana wa Israeli na mtandao wa giza kwa njia ya uzinzi. Alitumia kizazi cha
Moabu kutokana na historia ya chimbuko la Moabu lilivyokuwa – Mwz 19:30-38. Na
ndicho anachokifanya leo.
6. Baal
– 1 Falme 18:25 –
26 – baal ni mungu wa wafilisti aliyemfanya Yezebeli kuwa Malkia wake katika
ulimwengu wa giza – 1 Falme 19 : 1 – 2 upako wa kishetani wa Yezebeli,
ulitiririka kutokakwa Malkia wa baharini na Malkia wa Pwani. Baal ndiye alikuwa
nembo kuu ya miungu yote ya wafilisti.
·
Roho
za miungu hii bado zinatenda kazi hata sasa, lakini kwa mchepuo wa tofauti.
Bila neno la ufunuo siyorahisi kugundua.
·
MIJI 5 YA WAFILISTI – YOSHUA 13:2-3
1. Gaza
2. Ashdodi
3. Ashkeloni
4. Gathi
5. Ekroni
Nguvu za uharibifu wa
kipepo zilikuwa zinatokea katika miji hii. Mawimbi ya giza yalirushwa toka katika miji hii.
Kulikuwa na nguvu ya pamoja iliyotoka kwenye muungano wa miji hii katika
ulimwengu waroho. Ni vema kujua, nguvu unayopambana nayo inatoka katika mji
gani/nchi gani.
·
Viongozi waliopewa upako wa kutawala
miji hiyo 5.
Kidemokrasia au kisheria hata
kisiasa – waliitwawakuu wa miji, na mashehe watano wa wafilisti – Yoshua 13:3
neno Mashehe, katika nyakati zetu lisitafsiriwe vibaya, kwani tokea mwanzo
lilimaanisha kama kiongozi wa mji aliyepewa heshima. Kwani hata Nehemia
mtumishi wa Mungu aliye hai - alilitumia
kwenda kuwaambia viongozi Fulani ili wafanikishe kazi ya Mungu wa kweli – Neh
4:14. Viongozi wa miji hiyo 5 katika ulimwengu wa roho walitambulika kama wakuu
wa giza wanaotenda kazi kwa mkusanyiko wa nguvu ya pamoja. Wana harakati wakuu wa
milango ya kuzimu, pia walikuwa wakuu wa mila na desturi. Walihusika kwa kila
tukio lililohusiana na watumishi wa Mungu katika kilele cha vizuizi na
upinzani.
·
Kila
miji unayoiona katika bara la Africa miungu imeweka wakuu wa hiyo miji katika
namna ya usiri mkubwa, ilikuachilia nguvu za giza katika Nyanja tofauti
tofauti.
·
Kwa
sababu hiyo, kuna ulazima wa kuzingatia ukweli kwamba, maombi yako yafuatane na
mji uliopo. Yaani kuomba kwako kuungane na hekima ya kushughulikia ulimwengu
waroho wa mji wako. Usisahau hilo.
MAELEKEZO
1. Dagoni
2. Maashtoreth
3. Beth – shan\baal – zebubu
4. Baal – peori
5. Baal
·
Jifunze
kufanya maombi kwa kushughulikia roho za miungu hii zinazopunguza spidi za
maendeleo yako kiroho na kimwili. Piga miungu hiyo katika ulimwengu wako wa
maombi, mpaka inaposalimu amri, ifurumishie mawe ya moto mpaka inapotoroka.
MAOMBI
1. Damu ya yesu kristo, peleka kizaazaa
kwenye miji mitano ya kiroho iliyoungana kwa ajili ya kuunda nguvu ya panoja ya
kunimaliza – katika jina la Yesu kristo.
2. Roho mtakatifu – sababisha
mahangaiko na vifo vya ghafla kwa wakuu wa giza watano walioungana kwaajili ya
kukomesha na kuimaliza hatma yangu - katika jina la Yesu kristo.
3. Mungu Baba Mungu Mwana Mungu Roho
mtakatifu ifungue nafsi yangu isiendelee kushikiliwa na miungu ya kigeni kwa
namna yoyote nisiyoijua - katika jina la Yesu kristo.
4. Moto wa Mungu vunja pingu za miungu
ya wafilisti kwenye mikono na miguu yangu - katika jina la Yesu kristo.
5. Miungu mnaoleta milango ya kuzimu
nyumbani kwangu mpigwe mweleka na nguvu za moto ulao mnikimbie mara moja -
katika jina la Yesu kristo.
v ONYO!!!
Umekatazwa kutoa copy ujumbe ulioko
kwenye karatasi hii ili kumpa mwingine,isipokuwa umeruhusiwa kumchukulia rafiki
yako karatasi yake mwenyewe. Itakuwa dhambi ya makusudi ya kutokutii usipo
zingatia onyo hili.
AMINA!!!!.
Comments
Post a Comment