MFULULIZO WA MAFUNDISHO YA APOSTLE ALAM J. KAYENGELA KWENYE KONGAMANO LA SIKU NANE ARUSHA TANZANIA (TAREHE 5-12 MWAKA 2013)
SIKU YA 6:
·
MIUNGU NA MAKABILA YA VIZAZI VILE.
Miungu ilisonga mbele kwa makusudi
makuu kwenye mzunguko wa ulimwengu wa makabila.
·
Baadhi ya miungu na harakati zake
juu ya makabila 2Falme 23:13.
1. Ashtoreshi – alikuwa mungu mke wa kabila la
wasidoni, kama inavyoonekana katika 1 Walue 11:33. Ashtoreshi ni kirefu cha
“Ashera” ambaye pia aliaminiwa kuwa ni mungu anayefanikisha uzazi wa kila kitu.
2. Kemoshi
– alikuwa mungu wa
wamoabi – mungu kemoshi na baal – peori ni miungu iliyowatesa sana kabila la
moabi hata kwa kuwafanya kuwa waasherati na wazinzi – Hesabu 25:1 – 3.
3. Milkomu
au moleki – alikuwa
mungu wa Amoni. Moleki alilitawala na kulikandamiza kabila la waamoni. Mungu
moleki ndiye aliyelifanya kabila la waamoni kuamini kwamba, wakitoa sadaka ya
kafara ya watoto watafanikiwa na kuwa karibu na mungu – Lawi 20:1 – 5 na 2Falme
17:17 ndiye anayeongoza ibada za kafara za watoto mpaka leo, na kafara za mimba
changa. Sulemani alipomuoa mke wa Amoni bila kujua miungu ya chimbuko lake,
ghafla nafsi yake ilinaswa katika ulimwengu wa giza na akaanza kujenga
madhabahu kwa ajili ya mungu Moleki. Na kuanzia hapo miungu 4 ilianza kummiliki
– 1Falme 11:5 -7.
·
Unaposoma 1Falme 11:5-8
-
Unagundua
kuwa, nafsi ya Mfalme Sulemani ilifungwa pingu na miungu 4.
1. Ashtoreshi – mungu mke wa wasidoni
2. Milkomu au moleki – mungu wa Waamoni
3. Kemoshi – mungu wa Wamoabu
4. Baal – miungu ya Wafilisti ambayo
aliitolea sadaka.
·
Undani wa makabila ya vizazi vile
-
Miungu
hushughulika sana na vichwa vya makaabila au wakuu wa makabila – mfano: Mwa
49:3-4 Rubeni alipozini na mke wa baba yake – aliharibu hatima ya kizazi chake
– Kutoka 6;14 1Nyakati 5:1-3 watoto wake wanne yaani Hanoki, na Palu na Hersoni
na Karmi – Baraka zao zilienda kwa Yusufu – 1 Nyakati 5:1. Huwezi ukajua leo
kichwa cha kabila lako au mkuu wa kabila lako alifanya nini na Mungu au miungu,
lakini unaweza kusoma alama kwa kuona matokeo ya maisha uliyonayo.
·
Pingu za kabila
-
Chunguza
vizuri katika Amosi 1:6-8 – Hapo unaona kabila zima limepigwa pingu na kufungwa
kisha kutiwa katika mikono ya Edomu (roho ya kuhangaika na kufa vibaya) nguvu hiyo
ya kulifunga kabila zima ilitoka kwenye kati ya miji ile 5 ya wakuu wa
Wafilisti (wakuu wa giza) waliokuwa wanatawala miji mitano ya wafilist. Kwa
hiyo kabila zima lilifungwa kwa upako wa giza ulioachiliwa kutoka kwenye miji 4
ya wakuu wa giza – yaani, Gaza, Ashdodi na Ashkeloni pamoja na Ekroni.
-
Miungu
iliweza kulifunga kabila zima. Je! Iliwezekanaje kukamata kabila lote na
kulifunga? Kwa kupitia mtu mmoja (mkuu wa kabila) miungu ikalifunga
kabila.
·
Viapo vya kabila
Unaposoma vizuri katika Habakuki –
3:9 unaona wazi kwamba kuna viapo vya kabila au makabila. Sasa hatima yako
inategemea kiapo alichofanya mkuu wa kabila lako. Aliapa kumtumikia Mungu wa
kweli au miungu mingine? Katika bara la Africa makabila mengi na koo nyingi
wakuu wao waliapa kwa makusudi kujitoa nafsi zao kwa miungu ya kipepo.
·
Miungu
na makabila ya vizazi vile, ni jambo muhimu linalopaswa kuhamasisha fahamu zako
binafsi kugundua ukweli kwamba upo umuhimu katika kizazi chako leo kujitahidi
kujua namna ya kutumia nguvu ya mungu wa kweli, dhidi ya miungu ambayo kwa siri
kubwa imefanikiwa kupoozesha kanisa hasa kupitia makabila.
·
MAOMBI
1. Ee Mungu wa mipango mema juu yangu,
nakupa sifa na shukurani kwa kuwa umenifanya kuwa wa uzao wa Ibrahim na wa
kabila la simba wa Yuda kwa kupitia mpendwa Yesu Kristo. Kwa sababu hiyo
ninaikiri Damu ya Yesu Kristo juu ya kabila langu la zamani ambalo miungu yake
haikomi kunifuatilia. Miungu ya kabila langu la zamani nilipokuwa sijaokoka
nawapigia makofi ya kuwachanganya na kuwapotosha milele (piga sasa kwa nguvu
unapoendelea na maombi haya). Pingu za miungu ya giza mlionifunga kupitia
kabila langu moto ukukate kama uzi unavyokatwa na moto. Pingu za mapepo kutoka
kwenye chimbuko langu la kuzaliwa katika ukoo na kabila langu niache mara moja,
pigwa na malaika wa vita – Katika Jina la Yesu Kristo.
Katika
jina la Yesu Kristo, nasimama kinyume na viapo vya uharibifu walivyofanya wakuu
wa kabila langu kwa miungu ya kishetani – Katika Jina la Yesu Kristo.
Ninakataakuathiriwa na viapo walivyofanya
wakuu wa ukoo wangu, wakuu wa kabila langu, wakuu wa mji wangu, wakuu wa
kitongoji changu – kwa Jna la Yesu Kristo.
MAELEKEZO
1. Yale ambayo wazee wako hawakufanya
kwa Mungu wa kweli – wewe yafanye kwa bidii, ili usiweze kurudi kwenye pingu za
miungu ya kipepo.
2. Usisahau katika kipengele hiki
unapoomba,omba ukiwa unapiga makofi kwa nguvu utaona kila wakati upako waRoho
mtakatifu ukiisumbua miungu inayokusumbua.
v ONYO!!!
Umekatazwa kutoa copy ujumbe ulioko
kwenye karatasi hii ili kumpa mwingine,isipokuwa umeruhusiwa kumchukulia rafiki
yako karatasi yake mwenyewe. Itakuwa dhambi ya makusudi ya kutokutii usipo
zingatia onyo hili.
AMINA!!!!.
Comments
Post a Comment