MFULULIZO WA MAFUNDISHO YA APOSTLE ALAM J. KAYENGELA KWENYE KONGAMANO LA SIKU NANE ARUSHA TANZANIA (TAREHE 5-12 MWAKA 2013)
SIKU YA 7:
·
KAZI ZA MIUNGU YA WAFILISTI.
1. Kufuatilia na kuvizia watu maalumu
waliokabidhiwa kitu maalumu na Mungu.
-
Hili
linapaswa liwe onyo muhimu hasa kwa watu Fulani waliokabidhiwa jukumu maalumu
na Mungu. Umuhimu wa jambo hili, hatuwezi kuuelewa kwa ukamilifu kwa akili zetu
hizi za kibinadamu zilizojaa ubinadamu. Kufuatilia na kuvizia watu maalumu
waliokabidhiwa kitu maalumu na Mungu ni moja ya vipaumbele vya shughuli za
miungu ya wafilisti. Mfano Mfalme Sauli
kwa mashimo makubwa mawili, miungu ilifanikiwa kummaliza.
1.
shimo la kukosa uvumilivu wa kiimani – 1
Samwel 13:8 – 14 – shimo hilo linatafsiriwa
kama upambavu mbeleza Mungu – Mst 13
matokeo yake ni kunyang’anywa kile
ulichokuwa umepewa na atapewa mwingine Mst
14.
2. Shimo
la kukosa utii wa uaminifu – 1 Sam 15:1- 23 katika ulimwengu war oho shimo hili
linatafsiriwa kama – uovu – Mst 19 na
uchawi – Mst 23 – ndipo hali hiiinakupofusha macho usione kosa pale unapokosea
bali ujihesabie haki – Mst 19 – 20. Aliambiwa “Umekosea” Akajibu “Hapana
nimetii” Hakuliona kosa.
Mashimo haya mawili ya milango
ya kuzimu ya miungu ya wafilisti yalifanyika kuwa pingu na tanzi ya kummaliza
Mpakwa mafuta maalumu wa Mungu – 1 Samweli 10:1. Wafilisti wakiwa na uvuvio wa
nguvu za miungu, wakamfuatilia sana Sauli kwa umakini bila makosa, vita vikawa
vikali sana mpaka “WAKAMPATA” – 1 Samweli 31:1-3 Sauli
alijiua kimwili lakini akiwa ameshakamatwa kwenye ulimwengu waroho – 1Sam
31:3-5 – Wafilisti baada ya kumpata Sauli wakafanya sherehe na kuitukuza miungu
yao iliyofanikisha kukamatwa kwake – 1Samweli 31:8 – 10 – ukawa mwisho wa mtu
huyo maalum.
·
Mfano
wa pili – Samsoni mtu maalumu wa Mungu
-
Samsoni hakuwa mlokole wa kawaida hapa
duniani bali alikuwa maalumu aliyekuwa na kitu maalumu. Umaalumu wake unaonekana
kuanzia kwenye chimbuko lake la kuzaliwa – Waamuzi 13:1-25. Chimbuko la ukoo
wake wa kikabila alikuwa wa ukoo wa Dani – Mst2. Alikuwa mnadhiri toka tumboni
– maana yake alikuwa “Maalumu – Mst7”. Aliinuliwa na Mungu ili awe mwamuzi wa Waisraeli. Akatumikia
kusudi hilo yapata miaka ishirini -Waamuzi 16;31 (b).
Miungu ilikuwa
mbioni kumfuatilia mtu huyu maalum wa Mungu kupitia Wafilisti – Waamuzi 16:2
kwa mara ya kwanza Samsoni akafaulu kukwepa – Mst3. Lakini haikuchukua muda
tayari alikuwa amekamatwa Mst 21, ili kumfanya awe dhaifu zaidi kitu cha kwanza
waling’oa macho yake – Mst 21. Hakukamatwa na Wafilisti pekee bali ilikuwa
miungu hiyo, ikawa nilazima Wafilisti kuitolea sadaka ya shukrani miungu hiyo –
Mst23- 24. Mungu Dagoni ndiye aliyeendesha oparesheni hiyo ya kukamatwa kwa
Samsoni Mst 23. Usifanye
mchezo na miungu unahitaji kuongeza umakini wa kujua namna ya kutumia nguvu ya
Mungu dhidi ya miungu.
·
Mfano wa tatu ni
Yesu Kristo – Japo
alikuwa mtu maalum wa Mungu, kwa ukaribu sana alifuatiliwa na kuviziwa sana –
Luka 20:21. Katika Agano jipya – Yesu alikuwa anaviziwa na nguvu tatu kubwa za
miungu – Beelzlzebuli yaani Mkuu wa mapepo – Math 12:23 – 24 na Apolioni au
Abadoni ambaye ni Malaika wa kuzimu- Ufunuo 9:11 pamoja na Mfalme wa uweza wa
anga – Efeso 2: 1-3 Bwana Yesu alishinda miungu hii kwa jinsi alivyotembea na
misingi 4 ya kiroho ambayo nitakuwa naifunua kesho kwa uwezo waRoho mtakatifu 1
Korinto 2:10.
2.Kufukia na kugombania mipenyo yako
- Hii ndiyo kazi ya
miungu ya Wafilisti, inafanya juhudi ya hali ya juu ili kufukia na kugombania
upenyo wako. Angalia mfano kwa Isaka – Mwz 26:15 – 22.
1. Wafilisti
walinyang’anya kisima – Mwz 21:25
2. Wafilisti
wakagombania kisima – Mwz 26:18 - 22
3. Wafilisti
walifukia pia kisima – Mwz 26 : 15
Miungu ya Wafilisti
ilimfuatilia Isaka kwa namna hiyo, hasa kwa upande wa uchumi – akawa ameishinda
na akawa mkuu – Mwz 26:12 – 14 hakutaka kushindwa.
3.
Miungu inasababisha
Mungu asikujibu kwa sauti ya wazi, kwa ndoto na urimu – 1Sam 28:6
a. Sauti ya wazi ni
nini? – ni ile sauti unayoweza kusikia hata kwa masikio haya ya kawaida –
Matendo 13:2-3 n.k
b. Sauti ya ndoto ni
nini? – ni vile Mungu anavyoweza kuku ambia au kukuonyeshakitu ukiwa umelala
usingizi mzito – Ayubu 33:14 – 15.
c. Urimu ni nini? –
Kutoka 28:15 – 30, Hesabu 27:21na 1Samweli 14:41 pia na Ezra 2:63 – kwa hiyo, urimu
ni kitu kilichotumiwa na kuhani mkuu au kiongozi mkuu kwa ajili ya kutafuta
jibu la hapana au ndiyo kwa Mungu –kwahiyo kuhani mkuu alipotumia urimu
kwaajili yakupata jibu la hapana au ndiyo kwa Mungu alifanya nfano unavyoweza
kuchukua sarafu mbili kabla ya kuzirusha juu kwa pamoja, unamwambia Mungu
kwamba, ikiwa sarafu hizi zitaonyesha namba- jibu litakuwa ni NDIYO ikiwa
zitaonyesha sura ya picha jibu litakuwa ni HAPANA ikiwa moja itaonyesha namba
na nyingine sura ya picha – jibu litakuwa ni HAKUNA JIBU, kwa hiyo baada ya
kutamka maneno kama hayo – kuhani huyo alirusha juu na kuangalia kile Mungu
atamwambia. Hiyo ni moja ya njia kubwa ambayo Mungu aliitumia ili kumjibu mtu
wake kwa ajili ya kuthibitisha jambo furani. Hicho ni kitu cha kawaida tu, kwa
sababu ni kama vile tu, unavyoweza kumuomba Mungu aina ya MAOMBI YA ISHARA –
Waamuzi 6:36-40 maombi haya ya ishara nimeyaelezea sana kwenye kile kitabu cha
AINA 90 ZA MAOMBI.
4. Kuondoa utukufu.
Unapookoka
– Bwana Yesu anaruhusu utukufu wa Mungu kuja juu yako – Yohana 17:22 mara moja
miungu huanza kukufuatilia ili kukuondolea huo utukufu. Unabaki mkavu bila
uwepo na nguvu ya Mungu. Fuatilia vizuri katika 1 Samweli 3:1-21, 4:1-22 na
5:1-12. Mungu Dagoni wa Wafilisti aliongoza oparesheni yakuondoa utukufu wa
Mungu wa Israeli kwa wana wa Israel. Ikabodi ina maa utukufu umeondoka. Baada ya
IKabodi kuondoka ndipo wana wa Israeli
wakapigwa sana na Wafilisti.
5.
Kuandaa milango ya
kuzimu
-
Katika
Mathayo 16:18 Bwana Yesu alisema kwamba milango ya kuzimu haitalishinda kanisa
lake. Kwa hiyo alionyesha wazi kwamba, kanisa linashindana sana na milango ya
kuzimu. Miungu inaandaaje milango ya kuzimu? Tazama kwenye Waamuzi 16:5 wakuu
watano wa Wafilisti walimuandaaDelila kama mlango wa kuzimu wakamkamata mtu
maalumu wa Mungu – Samsoni. Miungu kabla
ya kukumaliza, inatafuta kwanza kujua asili ya nguvu zako ni nini? Asili ya
nguvu za Samsoni ilikuwa kwenye nywele na hapo ndipo miungu ilienda kushughulikia.
Milango ya kuzimu ambayo ndiyo mikono ya miungu ya Wafilisti kazi yake ni
kukumaliza kwenye asili ya nguvu zako.
MAOMBI:
1. Roho Mtakatifu
naomba saa hii upigane na miungu yote iliyonizunguka katika ulimwengu waraho –
Katika Jina la Yesu Kristo.
2. Mawakala wa miungu
mnaovizia uhai wangu mpigwe butwaa nakuchanganyikiwa kisha mfe - Katika Jina la
Yesu Kristo.
3. Roho mtakatifu piga
moto kazi zote za miungu kwenye maisha yangu - Katika Jina la Yesu Kristo.
4. Kila oparesheni
kubwa na ndogo ambazo miungu wanafanya ili kunikamata na kunimaliza – Roho
mtakatifu kataa pamoja na mimi - Katika Jina la Yesu Kristo.
5. Roho mtakatifu
ifiche sura yangu wala miungu haitaniona kwenye Darubini zao - Katika Jina la
Yesu Kristo.
MAELEKEZO
1.
Rudi kule mwanzo wa somo hili, uchukue
mfano wa Mfalme Sauli utajua kwanini miungu ilimmaliza – hivyo wewe uwe makini.
v ONYO!!!
Umekatazwa kutoa copy ujumbe ulioko
kwenye karatasi hii ili kumpa mwingine,isipokuwa umeruhusiwa kumchukulia rafiki
yako karatasi yake mwenyewe. Itakuwa dhambi ya makusudi ya kutokutii usipo
zingatia onyo hili.
AMINA!!!!.
Comments
Post a Comment