MFULULIZO WA MAFUNDISHO YA APOSTLE ALAM J. KAYENGELA KWENYE KONGAMANO LA SIKU NANE ARUSHA TANZANIA (TAREHE 5-12 MWAKA 2013)
SIKU YA 3:
·
KUFUATILIWA NA WAMILIKI AU MMILIKI WA MIUNGU NA JINSI YA KUMSHINDA.
Mmiliki
wa miungu, ana cheo kikubwa sana katika ulimwengu waroho. Ni kwa sababu, chini
yake anatumikiwa na majeshi mengi ya mapepo. Kimo cha chini anakuwa na wastani
wa mapepo milioni 40. Yote yanatenda kazi kwa amri yake. Ana utisho usio wa
kawaida katika ulimwengu wa kipepo.
·
Nabii Eliya baada ya kuua manabii 450 wabaal waliokuwa wanamilikiwa na Yezebeli, mwanamke aliyekuwa mmiliki wa miungu – 1Falme
18:17 – 19, 22 na 36 – 40 mmiliki wa miungu huyu Yezebeli alitoa tangazo makini
kumwambia mtumishi wa Mungu ajipange kwa ajili ya kupambana naye kesho – 1Falme
19:1 – 3. Kwa kujua kile ambacho kilikuwa ni hakika kingemtokea – baada ya
taarifa hiyo, Eliya aliamua kukimbia. Akamkimbia Yezebeli.. ni siku chache tu,
Nabii Eliya alikuwa amewaua Manabii 450 wa kipepo. Aliwashinda 450 akiwa peke
yake lakini alimkimbia mmiliki wa miungu mmoja Yezebeli.
·
Mika asiyeokoka – mmiliki wa miungu kwa
kudhamiria kabisa aliwafuatilia wana wa Dani kwa juhudi kubwa huku akipiga
kelele – Waamuzi 18:11 – 31 kwa sababu nawao walikuwa wamiliki wa miungu
wakaonekana kuwa wana nguvu kuliko yeye akawa ameshindwa kwani walimtahadharisha
kwamba – ukiendelea kutupigia kelele zako hizo – uhai wako utaupoteza mara
moja. Alizingatia onyo hilo, na kunyamaza kimya.
·
Labani mmiliki wa miungu – kwa ghadhabu na
chuki alimfuatilia Yakobo – Mwz 31 : 22 – 35 ni kwa sababu Mungu alipunguza
spidi yake kwa kumwambia Labani kwamba, ajihadhari asimwambie Yakobo neno la
shari au la amani. Lakini hata hivyo hakuacha kumfuatilia Yakobo. Unaona wazi
kuwa, Mungu wa Yakobo asingeingilia kati, bila shaka Yakobo angeshindwa. Lazima
uwe na uhakika na Mungu wako kwa kila hatua unayoichukua.
·
Wamiliki
wa miungu wa mji wa Yoashi – kwa mioyo yenye madhara walimfuatiatilia kwa
umakini mtumishi wa Mungu Gidioni – Waamuzi 6:25 – 30 walifanya uchunguzi na
kupeleleza, wakagundua kwamba anayepaswa kufuatiliwa ni Gidioni.
·
Wamiliki
wa mawakala wa Artemi Mungu mke wa Efeso walimfuatilia na kumuanzishia ghasia
Mtumishi wa Mungu Paulo – Matendo 19 : 23 – 28, kwa sababu ya nguvu waliyokuwa
nayo mji wote ulitikisika hali ya hewa ya mji ikabadilika.
1. Yezebeli
2. Mika asiyeokoka
3. Labani
4. Wenyeji wa mji wa
Yoashi
5. Wamiliki na
mawakala wa Artemi mungu mke wa Efeso.
Hawa
ni moja ya mifano hai ya kukufanya wewe kuelewa kuwa, wapo wamiliki wa
miungu wanaofuatilia kanisa.
·
Siri
ya kuwashinda ni rahisi na nyepesi.
1. Usiwe muoga – kwa kuwa una uhakika
kwamba aliye ndani yako ni mkuu kuliko miungu iliyo ndani yao.
-
Eliya hakulikumbuka jambo hilo. Alikimbia.
2. Usiwe na kitu chochote cha miungu
kwenyemaisha yako (au vitu vilivyowekwa wakfu kwa miungu)
-
Hii inamaanisha, hata tabia mbaya –
imewekwa wakfu kwa miungu, mfano – ukorofi, wivu, hata kutokujali haki za
wengine. Hivyo vyote ni wakfu kwa miungu ukiwanavyo – lazima wamiliki wa miungu
watakuandama na kukupigia makelele yakiwemo magonjwa na wachawi.
3. Kwa kuwa wanaweza kuyamaliza kabisa
maisha yako kwa kukosa kwako umakini na usikivu.
-
Basi inabidi uwe wakfu kabisa kwa Mungu
mkuu ambaye jina lake ni BWANA WA MAJESHI na MTAKATIFU WA ISRAELI.
-
Uwe wakfu – maana yake ujitoe hasa kwa
kudhamiria na kuwa tayari kukabiliana na hatari yoyote ilimradi unatimiza
wajibu wa kumtumikia Mungu.
MAOMBI
1. Kila kamanda wa
kikosi na jeshi kubwa la miungu, Roho Mtakatifu atawasambaratisha mara moja
wakati nikiomba – kwa Jina la Yesu Kristo.
2. Giza kubwa toka mbinguni,
funika nyuso za wamiliki wa miungu wanaonifukuza katika ulimwengu wa Roho
katika Jina la Yesu Kristo.
3. Maombi yangu,
poozesha kabisa nguvu za wamiliki wa miungu wanaotumia vifaa vyao vya siri
kunyonya nguvu ya maombi ndani yangu – kwa Jina la Yesu Kristo.
·
Melekezo
1. Maisha ya
kujichanganya na dhambi kwa namna Fulani – mfano, kukosa uaminifu kwa namna
yoyote ile, uongo wa siku moja moja, tamaa ya uzinzi na malumbano ya kila mara
yasiyo na sababu kwenye familia – hayo yanaweza kukuweka kwenye nafasi ya
hatari sana – kwani unakuwa mahali ambapo,
mkuki wa wamiliki wa miungu unaweza kukupata muda wowote.
v ONYO!!!
Umekatazwa kutoa copy ujumbe ulioko
kwenye karatasi hii ili kumpa mwingine,isipokuwa umeruhusiwa kumchukulia rafiki
yako karatasi yake mwenyewe. Itakuwa dhambi ya makusudi ya kutokutii usipo
zingatia onyo hili.
AMINA!!!!.
Comments
Post a Comment