MFULULIZO WA MAFUNDISHO YA APOSTLE ALAM J. KAYENGELA KWENYE KONGAMANO LA SIKU NANE ARUSHA TANZANIA (TAREHE 5-12 MWAKA 2013)
SIKU YA 2:
MIUNGU NA CHIMBUKO LAKO
·
Harakati za miungu bado hazijapunguzwa
spidi bado zinasonga mbele kwa mwelekeo maalumu. Kwa kadiri usivyojua namna ya
kushughulika na chimbuko lako, ni kwa kadiri hiyo hiyo inavyokuwa vigumu
kuishinda miungu hasa iliyokuwepo katika mazingira ya chimbuko lako.
·
Kwa mfano – Moabu na kizazi chake.
-
Katika
2 Wafalme 23 : 13 na 1Walfalme
11 : 7 Moabu hakujua kwa nini – Kemoshi amekuwa Mungu wake. Hakujua. Alishituka
Mungu wake akiwa Kemoshi. Hata ikajulikana kote kwamba, Kemoshi ni mungu wa Wamoabu.
Mungu Kemoshi alimtenga Moabu na Mungu wa Israeli ambaye jina lake ni BWANA WA MAJESHI AU MOTO ULAO.
·
Mungu Kemoshi aliweza kumkamata na kumteka
Moabu kutokana na chimbuko lake. Hasa chimbuko la kuzaliwa.
-
Ukisoma vizuri katika Mwz 19 : 30 – 38 Lutu alikuwa na mabinti wawili (mkubwa na mdogo)
mkubwa akamshauri mdogo kwamba, wafuate desturi ya dunia yote ya uzinzi ili
kuleta uzao – Mst 31. Wana wa Mungu
aliye hai, tumezuiliwa kufuata desturi ya kidunia – Efeso 2 : 1 – 3, kwani kufanya hivyo kunakufanya uwe mwana wa
laana. Bila kujua, binti wa Lutu waliipitia njia hiyo wakatengeneza chimbuko la
laana. Pale walipozini na baba yao kwa makusudi. Nia yao ilikuwa nzuri lakini
imelaaniwa. Miungu ilifuatilia tukio hili kwa ukaribu sana.
-
Binti mkubwa wa Lutu akabeba mimba toka kwa
baba yake (mimba ya uziznzi) akazaa mtoto akamwita MOABU siku ileile Moabu
alipozaliwa, bila kuchelewa miungu ilikuwa tayari imemuwekea alama. Moabu ndiye
baba wa Wamoabi, kizazi chote na ukoo wote wa Moabu ulifunikwa na giza la
miungu kwa sababu ya chimbuko lake.
-
Binti mdogo wa Lutu naye alipobeba mimba ya
uzinzi akazaa mtoto na kumpa jina la Benami, ambaye ndiye baba wa Waamoni mpaka
leo.
-
Mungu alijifanya kama vile hazioni nyakati
hizo na akamzuia mtumishi wake Musa asije akayasumbua au kushindana na makabila
hayo mawili Kumb. 2 : 9 na Mst.19.
-
Mungu anazungumzia nini kuhusu kizazi cha
chimbuko la uzinzi? Ktk Hosea 2 : 4
anasema – sitawaonea rehema watoto wake, kwa maana ni watoto wa uzinzi –
Mtoto wa uzinzi au mtoto aliyezaliwa kwa uzinzi, hapati rehema asipoomba
rehema. Aombe rehema juu ya chimbuko lake.
·
Mahusiano
ya kitovu na chimbuko lako, Ezekieli 16 : 1 – 6.
1.
Siku ile uliyozaliwa kitovu chako hakikukatwa
– maana yake bado kimeunganishwa na chimbuko lako la asili. Inategemea wazazi
wako walikuwa na miungu gani wakati ulipozaliwa – lakini miungu ya chimbuko
lako inakukumbuka.
·
FANYA
MAOMBI HAYA:
1.
Ee Mungu Mtakatifu wa vizazi vyote unayejua
chimbuko langu tokea mbali, siku za kuzaliwa kwangu ulipita ukaniona nikigaagaa
katika damu yangu mwenyewe, sauti yangu ikuwasilie masikioni mwako kwa sababu
ya Damu takatifu ya Yesu Kristo iliyohai unirehemu kutokana na chimbuko langu –
katika Jina la Yesu.
2.
Damu ya Yesu Kristo – Safisha kabisa kitovu
changu leo – katika Jina la Yesu Kristo.
3.
Damu ya Yesu Kristo – Usiruhusu uovu wa
baba yangu na mama yangu kuniandama leo, kwa kuwa mtoto hatachukua uovu wa mzazi wake wala mzazi
hata chukua uovu wa mtoto wake– katika Jina Yesu Kristo.
MAELEKEZO:
1.
Mwambie Roho Mtakatifu akukwamue kule
ulikokwama kwenye chimbuko lako.
2.
Jifunze kuwa unafanya maombi mara kwa mara
– maombi yanayoshughulikia chimbuko lako na kitovu chako.
v ONYO!!!
Umekatazwa kutoa copy ujumbe ulioko kwenye karatasi hii ili
kumpa mwingine,isipokuwa umeruhusiwa kumchukulia rafiki yako karatasi yake
mwenyewe. Itakuwa dhambi ya makusudi ya kutokutii usipo zingatia onyo hili.
AMINA!!!!.
Comments
Post a Comment