MFULULIZO WA MAFUNDISHO YA APOSTLE ALAM J. KAYENGELA KWENYE KONGAMANO LA SIKU NANE ARUSHA TANZANIA (TAREHE 5-12 MWAKA 2013)
·
SIKU YA 1:
·
KUIFUNUA MIUNGU KWA UFAHAMU KATIKA AFRIKA NA ULIMWENGU WOTE.
Miungu
ni nini?
Ø Kwa ufupi na rahisi : miungu ni roho
isiyoonekana ambayo mara nyingi hukaa kwenye vitu vinavyoonekana – Mfano
Vinyago au Sanamu.
Labani - alimwambia Yakobo “mbona basi umeiiba Miungu yangu?” – Mwz 31 :
22 – 30 – akimaanisha vinyago – Mst
19.
Ø Miungu
ni roho zinazoishi katika usiri na nguvu, zinatenda kazi kwa ushirika wa
Majeshi mengi ya kipepo. Hazina haraka wala makosa katika kumdhibiti mtu.
Ø Miungu
inaweza kumhadaa mtu – kwamba anaweza kuimiliki wakati yeye ndiye mmlikiwa Mfano: Mwz 31 : 25 – 30 Labani, siku
zote alifikiri kwamba, ile miungu ilikuwa yak wake. Lakini kumbe yeye ndiye
aliyekuwa mali ya ile miungu. Hakuwa mmiliki wa miungu bali alikuwa mmilikiwa
wa miungu.
Ø Mika
asiyeokoka alimiliki miungu hata akaitafutia kuhani wa kuitumikia – Waamuzi 18 : 20 – 31 katika mwili, Mika
alimiliki miungu, katika roho miungu ilimmiliki Mika. miungu ilimuhadaa Mika. Tazama Mwz 35 : 2 na Mst 4 Yakobo
aliwaambia watu wake
“Ondoeni
Miungu migeni iliyoko kwenu………” Nao wakampa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa
mikononi mwao, na pete zilizokuwa masikioni mwao………”
Ø Miungu
ni roho zinazoweza kujificha kwenye, pete za masikioni (Heleni) kwenye kitu cha
mkononi – Mfano Saa, Bangili, Pete N.K. – ili mradi tu vitu hivyo vimewekwa
wakfu kwa miungu migeni.
1.
Heleni zilizo na miungu – kazi yake ni
kuziba sikio la ndani muhusika asishawishike kumsikiliza Mungu wala kumtii.
2.
Bangili, Pete au Saa zilizo na miungu ndani
yake – zitafunga mikono ya muhusika asiweze kupata mema ya Nchi kutoka kwa
Mungu wa kweli.
3.
Mavazi machafu waliyoambiwa watu wa Yakobo
– yalikuwa yale yaliyonajisiwa na Miungu – Mwz
35 : 2. Mavazi ya namna hiyo, Hukuondolea utukufu wa kweli wa ki Mungu.
·
Viwanda vingi vya nguo, Bangili, Pete,na
Saa, katika Bara la Africa, ni wakfu kwa miungu. Imekuwa vigumu kanisa kuleta athari
kwa shetani kwa sababu ya kumiliki vitu vilivyo na nguvu ya miungu bila
kuviweka wakfu kwa Mungu wa kweli.
·
Kujua miungu ni nini, itakuwa msingi na
hatua yako ya kwanza ya kutumia NGUVU YA
MUNGU DHIDI YA MIUNGU.
·
ELEKEZA
MOYO WAKO KWENYE MAOMBI:
1. Mshukuru Roho Mtakatifu kwa
kukufunulia ufunuo huu wa kuhusu jinsi ya kuifahamu miungu inayotesa Africa na
Ulimwengu kwa ujumla.
2. Mshukuru Roho Mtakatifu kwa sababu
anavyoifanya miungu ichanganyikiwe kwa ajili yako.
3. Mshukuru Roho Mtakatifu kwa jinsi
anavyoiharibu miungu iliyokuwa imejificha kwenye vitu vyako, kama – Nguo, Saa,
Bangili, Pete N.K.
4. Tangaza kwamba : Vazi lolote nililo nalo
ambalo limenajisiwa na miungu linalovuta matatizo kwenye maisha yangu
halitaniletea athari TENA, ninalilowesha
kwenye bwawa la Damu ya Mwana Kondoo Yesu Kristo.
v Maelekezo:
1. Kusanya vitu vyote ulivyo navyo,
uviweke wakfu na kuvitakasa kwa Damu ya Yesu.
2. Kila unaponunua kitu chochote, kabla
ya kukitumia – kiweke wakfu kwanza kwa Damu ya Yesu.
3. Tafuta nafasi nzuri – vipengele hivyo
4 vya maombi uvifanye kwa kufunga na kuomba.
v ONYO!!!
Umekatazwa kutoa copy ujumbe ulioko kwenye karatasi hii ili
kumpa mwingine,isipokuwa umeruhusiwa kumchukulia rafiki yako karatasi yake
mwenyewe. Itakuwa dhambi ya makusudi ya kutokutii usipo zingatia onyo hili.
AMINA!!!!.
Comments
Post a Comment