.....NENO LA UFUNUO LA WIKI KWA KANISA ULIMWENGUNI
Wiki hii ninaendelea na somo lilile la wiki iliyopita, pale tulipoishia
-->
-->KAMA HUJASHINDA MAUDHI;
-->
3.
LAZIMA UWE NA MOYO USIO PEPERUSHWA NA MAuDhI.
Mwanzo 45:5, Mathayo 5:10, Yohana 5:16, 15:20
2Tomotheo3:12, Galatia 4;29 na 1Kor 4:12 Lazima ufikie hatua ujue kustahimilia
maudhi. Kuwa na moyo usio peperushwa na maudhi, ni ilehali ya kujua kwamba maudhi
yapo yanapaswa kushindwa tu na siyo yakushinde.
Huwezi kuomba usikutane na maudhi, bali
unaweza kuomba kuyashinda maudhi.
Maudhi yasitazamwe kama kitu cha kuumiza
bali kama sehemu ya kukomazwa na kukuzwa kiroho.
![]() |
Mfano wa moyo ulio peperushwa na maudhi |
1.
Hutaweza kuishi na watu
popote pale
2.
Hutaweza kuwa mtumishi mwenye sifa za kweli
3.
Hutaweza kufika uzeeni
4.
Hutaweza kuikwepa Jehanam
5.
Hutaweza kufanya kazi na watu
kwa muda mrefu
6.
Hutaweza kudumu kwa muda
mrefu kwenye ndoa
7.
Hutaweza kuw na ushirika na
Rohomtakatifu
Kwa mafundisho haya na mengine mengi
wasiliana na Mtume Alam J.Kayengela. Kwa
ushauri na maombezi.
Comments
Post a Comment